Samia: Tutaendelea kushirikisha wadau kuwaletea maendeleo

NA MADINA ISSA

RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema ataendelea kushirikiana na wadau mbali mbali wakiwemo benki ya CRDB ambayo imekuwa mstari wa mbele katika kuisaidia serikali.

Akizungumza mara baaada ya kuweka jiwe na msingi soko la jamii la wajasiriamali kilichojengwa na Benki ya CRDB, alisema, benki hiyo imekuwa ikiisaidia serikali ambapo kwa mwaka jana wajasiriamali hao walitoa kilio hicho ambacho CRDB imelichukua hilo.

Alisema benki hiyo mara nyingi imekuwa ikiwashika mkono kuona maendeleo ya kusini yaliyoahidiwa yanatimia kwa wakati ambapo ndio lengo la tamasha hilo kupeleka maendeleo katika wilaya hiyo na mkoa kwa ujumla.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi gari mbili kwa uongozi wa Jeshi la Polisi Tanzania, Dk. Samia, alisema serikali imeamua kujenga vituo hivyo na kupeleka gari hizo na kuwasisitiza uongozi wa jeshi kuzitumia kwa lengo la kusaidia kurahisisha utendaji kazi zao katika suala zima la ulinzi wa raia na mali zao.

Alisema, kupatiwa gari hizo ni sehemu ya ufanisi wa kazi zao na sio kufanyia kazi nyengine na kuusisitiza uongozi wa jeshi la polisi kusimamia ili lengo liweze kufikiwa.

Mapema, akitoa taarifa kwa Dk. Samia, Mkurugenzi wa mawasiliano wa benki hiyo Tuli Mwambaka, alisema, wa benki ya CRDB, alisema, zaidi ya shilingi milioni 400 zitatuka katika ujenzi wa soko hilo ambapo zitakuwa na sehemu muhimu za kijamii ikiwemo vyoo ambapo pia wananchi wataweza .

Hivyo, benki hiyo kupitia foundation yake itajenga majengo yote na kuiomba serikali kuisaidia baadhi ya vifaa ili kuona lengo linafikiwa.

Nae, Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Hamad Khamis, alisema kukabidhiwa gari hizo zitawarahisishia ufanisi wa kazi zao na kuahidi kuyatumia kwa lengo lililokusudiwa.

Alisema, kipindi kirefu jeshi limekuwa na changamoto ya vitendea kazi Dk. Samia alipoingia madarakani alionesha nguvu kubwa ya kuboresha utendeaji kazi wa jeshi hilo ambapo lianza na majengo na sasa anaendelea katika usafiri kwa jeshi hilo na vyombo vya ulinzi na usalama.

Hivyo, alisema utoaji wa gari hizo ni kuonesha kwa vitendo dhamira yake kuwa yupo tayari kuisaidia vyombo vya polisi na kuwataka wananchi kwenda kuripoti kwenye vituo vya polisi endapo matokeo ya kihalifu na kusema vitendea kazi vipo vya kutosha na kuachana na majibu kwani usafiri sio tatizo na wanapopewa majibu hayo kuripoti kwa wakuu wa vituo.

Mapema, Dk. Samia, alifungua  ujenzi wa ukumbi wa mitihani na chumba cha kompyutakatika skuli ya sekondari Muyuni na  kufungua madarasa   sita skuli  ya Muyuni 

Pia aliweka jiwe la msingi  katika  skuli ya tasani, kuweka jiwe la msingi solo la jamii la wajasiriamali na kukabidhi  kituo cha polisi kizimkazi  mkunguni  na OCD mkunguni na  makunduchi na kituo cha mama  na mtoto kizimkazi dimbani.

Comments

Popular posts from this blog

ZALIRI, FLI zaingia makubaliano kuimariusha sekta mifugo

Ibueni changamoto zinazokamisha usawa wa kijinsia - Simbaya

Uislam unakubali uzazi wa mpango