ZMBF yawapelekea 'Tumaini Kits' wanafunzi wa kike

NA MWANDISHI WETU

MKE wa Rais wa Zanzibar, ambaye pia ni muasisi na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora (ZMBF), Mama Mariam Mwinyi, ameeleza kuwa taula za kike zinazotolewa na taasisi hiyo kwa wanafunzi wa kike zinawaweka kwenye mazingira salama.

Ameeleza hayo wakati wa hafla ya ugawaji wa taula za kike za Tumaini (Tumaini Kits) kwa wanafunzi wa skuli ya Kijini, iliyopo wilaya ya Kaskazini ‘A’, mkoa wa Kaskazini Unguja.

Mwenyekiti huyo alisema msichana anapotumia taula hizo huwa kwenye mazingira salama na kwamba muda wote humuwezesha kuhudhuria masomo yake bila ya kukatisha masomo kutokana na kuwa kwenye hedhi.


Mwenyekiti wa ZMBF mama Mariam Mwinyi akihutubia wakati wa hafla ya ugawaji wa taula za kike za Tumaini (Tumaini Kits) kwa wanafunzi.

Aidha alifahamisha kuwa taula za Tumaini kits zinazotolewa na ZMBF zina faida kwa wasichana na wanawake ikiwemo faida za kuwa salama kwa afya ya uzazi.

Alieleza kuwa zinaweza kutumika zaidi ya miaka mitatu na ni gharama nafuu tofauti na taula nyengine, huku pia zikiwa zinatunza usafi wa mazingira.


Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa taasisi ya ZMBF, Fatma Fungo akitoa taarifa ya utekelezaji wa kampeni ya hedhi salama wakati wa hafla ya ugawaji wa taula za kike za Tumaini (Tumaini Kits) kwa wanafunzi.

Mama Mariam Mwinyi alieleza kuwa ZMBF imehitimisha kampeni iliyoanza siku ya hedhi salama duniani iliyoadhimishwa kila ifikapo Mei 28 ya kila mwaka.

Alisema katika kipindi hicho chote had jana, ZMBF imekuwa ikigawa vifurushi vya tumaini ambapo kwa ujumla hapo jana zimegaiwa taula 562 kwa wasichana wa skuli za msingi na sekondari Kijini pamoja na skuli ya sekondari Potoa.

 

Mwenyekiti wa ZMBF mama Mariam Mwinyi akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini 'A', Sadifa Juma Kahamis na CEO wa taasisi hiyo, Fatma Fungo, wakiwa na badhi ya wanafunzi waliofikiwa na kampeni ya hedhi salama. 

Vilevile, Mama Mariam alitoa rai kwa wafadhili wa ndani na nje ya nchi kuiunga  mkono programu ya Tumaini Initiative ambayo ina lengo la kuwafikia wanafunzi 20,000 kwa mwaka.

Alisema hadi sasa programu hiyo imewafikia wanafunzi 1,557 walioko maskulini katika kipindi cha miezi mitatu minne kwa ushirikiano wa karibu wa wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali na Taasisi ya WAJAMAMA ambao ni wabobezi wa kutoa huduma na elimu ya afya ya uzazi.

Comments

Popular posts from this blog

ZALIRI, FLI zaingia makubaliano kuimariusha sekta mifugo

Ibueni changamoto zinazokamisha usawa wa kijinsia - Simbaya

Uislam unakubali uzazi wa mpango