Uislam unakubali uzazi wa mpango
NA MWAANDISHI MAALUM
KWA
muda mrefu, suala la uzazi wa mpango limekuwa na mjadala mrefu katika jamii na
vyombo vya habarijuu ya kama jee ni sawa au linapingana na maelekezo ya dini ya
Kiislamu?
Maelezo
yamekuwa mengi na yenye aina tafauti ya maelezo, lakini ukweli na uhakika ni
kwamba dini ya Kiislamu haina pingamizi juu ya uzazi wa mpango kwa vile
linasaidia mzazi na mtoto kuwa na afya bora.
Mjumbe wa Baraza la Maulamaa Zanzibar, Sheikh Khamis Abdulhamid, amesema dini ya Kiislamu haijakataza uzazi wa mpango ambao hauna na madhara kwa pande zote mbili.
“Wakati Quran inashushwa Masahaba waliwahi kusema Quran haikutukataza kutumia njia ya mshindo (kumwanga maji ya uzazi nje) ili kupanga uzazi“, Sheikh Khamis alisemaa.
Hata hivyo, aliongeza ni muhmu kwa wanawaume kujitahidi kufuatilia na kujipanga kupata elimu ili ndoa zao ziwe na furaha kwa kuweka utaratibu maalum wa kupata watoto.
“Ikiwa mtu atasema ukikataa kuzaa nimekuacha basi hakika hio ni talaka ila hilo sio lengo,maana unaweza kusema na mkeo akachoka akafanya yeye pekee yake mkawa mnaishi kwenye ndoa ambayo sio halali”, aliongeza.
Saida
Kassim (36) mama wa watoto sita mkaazi Magomeni, Unguja ni mama wa nyumbani
anayejishughulisha kupika badia asubuhi kwa ajili ya kujipatia riziki.
Muonekano
wa mwili wake ni wa mtu aliyechoka na dhaifu kidogo kwa sababu ya kupitia
changamoto kadhaa za uzazi.
Zaidi
ya hayo sasa anapambana na changamoto za malezi. Mtoto wake wa mwisho ni wa
umri wa miezi saba na aliyemtangulia ana
mwaka mmoja na miezi miwili
Tabaan
watoto hawa wawili bado hawajitambui
na wanamtegemea yeye kwa huduma zote,
kama kulishwa, kunyweshwa maji, kuoshwa na kadhalik. Usafi wa nyumba na
biashara yake ni mambo ya lazima kwamaisha yake na watoto wake.
Saida
anatamani kupumzika kuzaa ili apate muda wa kutosha kuwatunza watoto wake na
kurudisha hali yake ya mwili.
Lakini
amekabiliwa na kikwazo kikubwa. Nacho ni mume wako hataki kuliskia suala la
uzazi wa mpango kwa na licha ya kutotaka kulisikia.
Vile
vile ana hofu iliyotokanana na maneno yaliyozagaa kwenye jamii juu ya madhara
kadhaa yanayowapata wanawake wanaojiunga na uzazi wa mpango.
Mama
huyu wa watoto sita anasema mwenza wake hataki wawe na uzazi wa mpango wakati
hakuna kati ya watoto wake sita waliopishana miaka miwili kwenye kujifungua.
Kwa
maana hio huyu mama amekuwa akibeba mimba moja baada ya nyengineuda mfupi tu
baada ya kujifungua. Kwa mujibu wa tafiti nyingi na ushuhuda tunaouona katika
maisha hii ni hali hatarishi kwa mzazi na watoto wake.
“Mume
wangu hataki , anachotaka ni starehe na furaha
yake ni mimi kuzaa, sasa naogopa na nimechoka sana” amesema Saida kwa
sauti ya unyonge huku akiwa anamnyonyesha mtoto wake mdogo na mwengine
anamsubiri amhudumie.
Wakati
wa mazungumzo hayo, baba mzazi alikuwa hayupo na hapakuwepo mtu mwengine karibu
wa kumsaidia malezi.Ni hali ya kusikitisha.
Ni
dhahiri hali ya kutokukubaliana kwa pamoja kama familia inamrudisha nyuma Saida
kiafya na kiuchumi kwa familia.
Mama
huyo ameshindwa kufanya maamuzi sahihi ya kulinda afya na maisha yake kwa
sababu ya hofu ya kumuudhi mwenza wake, lakini zaidi kutokana na yeye na mmewe
kutopata elimu juu ya faida na furha iliopo katika uzazi wa mpango.
“Kwa
mfano nikipata mimba watoto wangu wanahangaika, maana mimi kila siku hospitali
kuumwa, Hivyo kwao wao kusoma ni shida na wakati mwengine hakuna mtu
anayewashughulikia watoto “, alieleza Bi Saida.
Ripoti
ya Afya ya Zanzibar ya mwaka 2022 inaonesha inaonesha matumizi ya uzazi wa mpango anzibar
yameshuka kutoka asilimia 7.5 (yaani
watu 75 kwa kila watu 1,000a) kwa mwaka 2020 hadi asilimia 6.9 ( yaani watu 69 kwa kila kwa
kila watu 1,000) kwa mwaka 2021.
Hii
inaashiria kuwepo kwa athari kubwa zaidi na hatari ya mama na mtoto kupoteza
maisha.
Juma
Mfaume Ali (32), Mwalimu wa sKuli ya Maandilizi binafsi iliyopo Magomeni anakiri kutokuwepo elimu ya afya ya uzazi kwa usahihi kwenye jamii.
Ameeleza
kuwa hali hii ipo zaidi kwa wanaume na aliwataka viongozi wa dini kuzungumzia
hali hii kwa upana wake na madhara yanayotokana na maamuzi ya upande mmoja, kama ya mume kushikilia
alitakalo.
“Haya
mambo hayasemwi kwa upana na athari zake kwa wanawake na kwa upande wa dini
kupanga uzazi kuaonekana jambo la kizungu wakati dini inatupa nafasi ya
kumpumzisha uzazi mwanamke kwa miaka miwili”, alieleza Juma.
Kwa
upande wake Daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake, Ummulkulthum Omar, alisema
taarifa za afya ya uzazi kwa wanafamilia kwa usahihi zinapatikana vituo vya
afya pale mama mjamzito anapoanza kliniki kwa wakati.
“Uzazi
wa mpango ni afya kwa sio familia ya mama au mtoto tu bali kwa ustawi wa jami
na nchi kwa jumla’, alisema.
Mradi
wa Afya ya Uzazi kwa wanawake na vijana umefadhiliwa na Shirika la Wellspring
Philanthropic Fund la Marekani ambapo kwa sasa unatekelezwa na Chama cha
Waandishi wa Habari Wanawake TAMWA kwa pande zote mbili za
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa lengo la kujenga uelewa wa jamii
juu ya umuhimu wa kufuata njia sahihi za uzazi wa mpango.
Comments
Post a Comment