ZBS yachangia kambi ya matibabu ya ZMBF
NA MWANDISHI WETU
TAASISI ya Viwango Zanzibar (ZBS) imeeleza kuwa itaendelea kushirikiana
na wadau mbali mbali ili kuimarisha ustawi wa jamii na uchumi kupitia njia
mbali mbali.
Yusuph alieleza kuwa hatua hiyo
inaangukia katika moja ya maeneo yanayosaidiwa na taasisi yake kupitia mpango
wa kusaidia jamii na wadau wake ikiwemo taasisi hiyo ambayo ni miongoni mwa
wateja wake.
“Kila mwaka huwa tunatoa sehemu ya mapato tunayokusanya kwa jamii na tumelkua tukipeleka msaada kwa wizara ya afya na kwa mwaka huu tunaelekeza sehemu ya mapato hayo katika tukio hili kuiunga mkono ZMBF lakini pia wizara ya afya”, alieleza Yussuph.
Hata hivyo aliahidi kuwa taasisi
yake itaendelea kusaidia shughuli za taasisi hiyo kupitia mpango wa kuimarisha
shughuli za ujasiriamali na kuishauri ZMBF kufanya kazi kwa karibu na taasisi
hiyo ili kuwasaidia wajasiriamali hasa wadogo.
Akipokea msaada huo kwa niaba ya
mwenyekiti wa bodi ya ZMBF, Mama Mariam Mwinyi, Ofisa Mterndaji Mkuu wa
Zanzibar Maisha Bora Foundation, Fatma Fungo, mbali ya kuishukuru ZBS, alieleza
kuwa msaada huo umekuja wajkati muafaka na kwamba utasaidia katika kambi hgiyoo
itakayofanyika Dole, wilaya ya Magharibi ‘A’, Unguja.
Alieleza kuwa kambi hiyo
itatanguliwa na matembezi ya kilomita tano yaliyolenga kujenga tabia ya watu
kupenda kufanya mazoezi kama sehemu ya mkakati ya kulinda afya na uchunguzi wa
maradhi mbali mbali pamoja na matibabu.
“Mtakumbuka mama Mariam (mke wa Rais
wa Zanzibar) kila mwezi alikua na matembezi yalilenga kuimarisha afya za
wananchi ikiwa ni miongoni mwa malengo ta taasisi yetu lakini sasa matembezi
yale tumeyaimarisha na tutayazindua rasmi Septemba 30, pamoja na kampeni ya
‘Afya bora, Maisha bora’”, alieleza Fatma.
Aliongeza kuwa katika kambi hiyo
wanatarajia kuwaona zaidi ya watu 3,000 ambao watafanyiwa uchunguzi na kupatiwa
matibabu ya magonjwa mbali mbali ikiwemo chanjo ya ugonjwa wa UVIKO 19, kisukari
na shinikizo la damu (presha).
Hata hivyo alitoa wito kwa wadau
kuendelea kuchangia kambi hiyo itakayoendeshwa na madaktari kutoka ndani na nje
ya Zanzibar chini ya usimamizi wa Wizara ya Afya na wananchi kujitokeza katika
matembezi hayo yanayotarajiwa kuanzia katika ofisi za Manispaa ya Magharibi
‘A’, Kianga.
Kwa mujibu wa ZMBF matembezi hayo
yaliyopewa jina la ‘Mariam Mwinyi Walkathon’ yanatarajiwa kuongozwa na mama
Mariam Mwinyi atakayeambatana na viongozi mbali mbali wa serikali, vyama vya
siasa, vikundi vya mazoezi, wajasiriamali na vikosi vya ulinzi na usalama
ambapo pia kutakua na uchangiaji wa damu.
Comments
Post a Comment