Mama Mariam ahimiza lishe bora, mazoezi kujikinga na maradhi

NA MWANDISHI MAALUM, LONDON

MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) mama Mariam Mwinyi, amesisitiza umuhimu kwa jamii kubadili mtindo wa maisha kwa kuzingatia lishe bora, sambamba na kufanya mazoezi.

MKE wa Rais wa Zanzibar, ambaye pia Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation, Mama Mariam Mwinyi akizungumza kwenye uzinduzi wa mpango wa utekelezaji wa afya za maradhi yasiyoambukiza (NCDs), hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Marlborough House nchini Uingereza.

Mama Mariam alitoa wito huo wakati wa uzinduzi wa mpango wa utekelezaji wa afya za maradhi yasiyoambukiza (NCDs) unaolenga kutekelezwa katika nchi 56 wanachama wa Jumuiya ya Madola katika ukumbi wa Marlborough House, Uingereza.

Alieleza kuwa ili kukabiliana na maradhi yasiyo ya kuambukiza kama ya saratani, ugonjwa ya moyo, shinikizo la damu na mengineyo hususani kwa vijana, kuna hitajika jamii kuhakikisha inapata lishe bora.

MKE wa Rais wa Zanzibar, ambaye pia Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation, Mama Mariam Mwinyi (kulia) akifuatilia mazungumzo wakati wa uzinduzi wa mpango wa utekelezaji wa afya za maradhi yasiyoambukiza (NCDs), hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Marlborough House nchini Uingereza

Alisema lishe bora ni muhimili muhimu unaoweza kujenga mwili kuwa na afya, ambapo pia katika kuepuka maradhi hayo yasiyo ya kuambukiza kuna umuhimu wa kufanya mazoezi.

Alisema maradhi yasiyo ya kuambakiza limekuwa janga kubwa ulimwenguni ambapo takwimu zinaonesha kuwa vifo vitokanavyo na maradhi hayo takribani asilimia 75 ya vifo vinavyotokea duniani.

Aidha mama Mariam alieleza kuwa serikali ya Mapinduzi Zanzibar na ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, zinachukua jitihada mbalimbali za kuimarisha sekta ya afya hususani afya ya mama na mtoto ili kupunguza hatari na vifo vya kundi hilo.

Alizitaja jitihada hizo kuwa ni pamoja na ujenzi wa miundombini ya kisasa ya kutolea huduma za afya, upatikanaji wa vifaa tiba, dawa na rasilimali watu yenye ujuzi na utaalamu wa kukabiliana na maradhi yanayoambukiza na yasiyoambukiza.

Kando ya mkutano huo, Mama Mariam, aliyeambatana na Waziri wa Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Riziki Pembe Juma, alikutana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Patricia Janet Scotland.

Katika mazungumzo yao, mama Mariam na katibu huyo walizungumzia ushirikiano kati ya jumuiya hiyo na ZMBF kupunguza vifo vitokanavyo na magonjwa yasiyoambukiza na kumaliza vitendo vya ukatili wa kijinsia kupitia programu ya Jumuiya ya Madola ya ‘Says No More’.

Comments

Popular posts from this blog

ZALIRI, FLI zaingia makubaliano kuimariusha sekta mifugo

Ibueni changamoto zinazokamisha usawa wa kijinsia - Simbaya

Uislam unakubali uzazi wa mpango