Mkakati, mpango kazi kuimarisha mianzi wazinduliwa

NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki, amezindua mkakati wa uimarishaji wa miti ya mianzi na kueleza kuwa tafiti zimebaini kuwepo kwa takribani hekta milioni 12.5 zinaweza kuuteshwa miti hiyo nchini ili kuzuia mmomonyoko wa ardhi na kunyonya hewa ukaa. Amesema utafiti huo unaonesha Tanzania inapoteza eneo la misitu yenye ukubwa wa hekta zaidi la 469,000 kila mwaka, hali ambayo sio nzuri na halikubaliki hivyo juhudi za pamoja zinahitajika. Kairuki alieleza hayo jana wakati akizindua mkakati wa kitaifa wa mianzi na mpango kazi wa mkakati huo uliofanyika katika Chuo cha Taifa cha Utalii, Dar es salaam. Alisema miti ya mianzi ina nafasi kubwa katika uhifadhi wa mazingira kwa kufyonza hewa ya ukaa (carbondioxide) kwa zaidi ya mara 40, hivyo zao hilo ni muhimu katika utunzaji wa mazingira na kupunguza athari za mabadiliko ya Tabianchi. WAZIRI Kairuki akiwa na Katibu Mkuu Abbas, Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya bunge ya Ardhi, Mal...