Dk. Khalid ashajihisha mashirikiano kufikia uchumi wa kidigitali

NA MWANDISHI WETU

WADAU wa sekta ya mawasiliano na mitandao nchini wametakiwa kuimarisha ushirikiano na mamlaka za serikali ili azma ya mageuzi ya kidigitali ifikiwe.

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, Dk. Khalid Salum Mohammed, (pichani), ametoa wito huo katika hafla ya uzinduzi wa ushirikiano wa kibiashara kati ya kampuni ya mawasiliano ya Airtel Tanzania na kampuni ya usambazaji wa maudhui ya Zanzibar Cable Television (ZCTV) iliyofanyika katika hoteli ya Golden Tulip, Uwanja wa ndege, Zanzibar.

Dk. Khalid alieleza kuwa serikali zote mbili za Tanzania, zimewekeza miundombinu na mazingira rahisi ya kuwezesha taasisi na kampuni za mawasiliano kutekeleza majukumu yao kwa faida.


Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, Dk. Khalid Salum Mohammed, (katikati),  akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa masirikiano ya kibiashara kati ya Airtel Money na ZCTV.

Aliongeza kuwa hatua hiyo inalenga kuleta unafuu wa gharama za mawasiliano kwa wananchi lakini pia kurahisisha upsatikanaji wa huduma mbali mbali zikiwemo za kifedha.

“Katika kipindi cha miaka mitatu, serikali imeimarisha uwezo wa mkongo wa taifa kuhudumia watoa huduma za mawasiliano lakini pia minara zaidi ya 40 imejengwa katika maeneo mbali mbali ya Unguja na pemba, lengo likiwa ni kurahisisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano”, alieleza dk. Khalid.

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, Dk. Khalid Salum Mohammed, (katikati),  akipokea kifaa cha mtandao wa intaneti toka kwa Mkurugenzi wa Airtel Money, Andrew Rugamba, wakati wa uzinduzi wa masirikiano ya kibiashara kati ya Airtel Money na ZCTV.

Aidha alizipongeza taasisi hizo kwa kuonesha mfano na utayari wa ushirikiano katika kukuza biashara na upatikanaji wa huduma jambo litakalowasaidia wateja wao lakini pia kuimarisha uchumi wa nchi.

Alieleza kwamba serikali inahimiza ushirikiano baina yake na sekta binafsi na inapotokea taasisi binafsi zinaungana na kushirikiana kwa lengo la kuimarisha hduma, kuna uwezekano mkubwa wa kufanikisha malengo ya nchi kukuza uchumi wa kidigitali.

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, Dk. Khalid Salum Mohammed, (katikati),  akipokea king'amuzi cha ZCTV toka kwa Kaimu Mkurugenzi wa ZCTV Khafidh Kassim, wakati wa uzinduzi wa masirikiano ya kibiashara kati ya Airtel Money na ZCTV.

Awali Mkurugenzi wa Airtel Money, Andrew Rugamba, alieleza kuwa kampuni hiyo mimelenga kurahisisha shughuli za kifedha ili kujenga tabia ya watumiaji wa huduma zao na wananchi kwa ujumla kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha lakini pia ujumuishaji wa kifedha.

Alieleza kuwa kupitia ushirikiano kati yao, wateja wa ZCTV watakuwa na uwezo wa kulipia huduma za ving’amuzi kupitia huduma za kifedha za kampuni hiyo (Airtel money) bila ya kwenda katika vituo vya kutolea huduma vya kampuni hiyo.

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, Dk. Khalid Salum Mohammed, (katikati),  Kaimu Mkurugenzi wa ZCTV, Khafidh Kassim na Mkurugenzi wa Airtel Money, Andrew Rugamba wakiwa na wafanyakazi wa Airtel Tanzania wakati wa uzinduzi wa masirikiano ya kibiashara kati ya Airtel Money na ZCTV.

“Baada ya kuimarisha huduma zetu na kuzindua mtandao wa kasi ya 5G, tumeongeza huduma zinazotolewa zikiwemo za kifedha ambapo sasa tunarahisisha huduma za malipo kama ya ada za shule na kwamba tumedhamiria kufanya mambo makubwa hapa Zanzibar katika siku za usoni”, alieleza Rugamba.

Aidha aliipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji yanayochochea kasi ya ukuaji wa uchumi nwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, Dk. Khalid Salum Mohammed, (katikati),  Kaimu Mkurugenzi wa ZCTV, Khafidh Kassim na Mkurugenzi wa Airtel Money, Andrew Rugamba wakiwa na wafanyakazi wa Zanzibar Cable Television wakati wa uzinduzi wa masirikiano ya kibiashara kati ya taasisi hizo.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi mkuu wa zctv, hafidh kassim hafidh, alieleza kuwa mafungamano hayo yanalenga kuwarahisishia kufanya malipo wateja wao kwa kufanya miamala ya kifedha kulipia huduma bila ya kufika kwenye vituo vyao vya mauzo.

Alieleza kuwa hatua hiyo mitapunguza misongamano kwenye vituo hivyo na kuokoa muda wa wateja wao na kwamba aliahidi kuimarisha huduma zikiwemo za mtandao wa intaneti katika siku za usoni.

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Dk. Khalid Salum Mohammed (katikati) akisalimiana na Mkuu wa Biashara wa Airtel Tanzania kanda ya Pwani, Mussa Sultan, alipowasili hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa ndege Zanzibar kushiriki uzinduzi wa mahusiano ya kibiashara kati ya kampuni ya Airtel Tanzania na Zanzibar Cable Television . Kulia ni Mkurugenzi wa Airtel Money Andrew Rugamba.

Aidha alimshukuru waziri huyo na watendaji wa wizara yake kwa kusimamia vye sekta ya mawasiliano na kuahidi kuwa wataendelea kushirikiana na wadau mbali mbali kufanikisha malengo ya taasisi hiyo.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na wadau wa sekta ya mawasiliano, elimu na habari akiwemo naibu katibu mkuu wa wizara ya ujenzi, mawasiliano na uchukuzi, Mhandisi Shomari Shomari, Meneja wa huduma za Airtel Money, Mariam mwamnyalla, alieleza kuwa kampuni hiyo imetanua wigo kwa kuwa na mawakala 220,000 Tanzania nzima.


Mkuu wa Biashara wa Airtel Tanzania kanda ya Pwani, Mussa Sultan (kushoto), akimsikiliza Mkurugenzi wa Airtel Money, Andrew Rugamba, kabla ya uzinduzi wa mahusiano ya kibiashara kati ya kampuni ya Airtel Tanzania na Zanzibar Cable Television uliofanyika hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa ndege Zanzibar. 

“Kampuni ya Airtel Tanzania ni mali ya Watanzania kupitia Msajili wa hazina anayemiliki hisa asilimia 49 huku airtel afrika ikiwa na asilimia 51 na ndio maana mara zote tunalenga kuwafikishia watanzania huduma bora mahali walipo”, alieleza Mariam.

Hivyo alitoa wito kwa watanzania kuchangamkia fursa zilizopo zikiwemo za bima ya afya, mikopo nafuu na ubia katika sekyta ya kilimo sambamba na huduma za malipo kidigitali kwa ajili ya kuokoa muda.  

WAGENI waalikwa wakifuatilia uzinduzi wa ushirikiano wa kibiashara kati ya Airtel Money na Zanzibar Cable Television





  

Comments

Popular posts from this blog

ZALIRI, FLI zaingia makubaliano kuimariusha sekta mifugo

Ibueni changamoto zinazokamisha usawa wa kijinsia - Simbaya

Uislam unakubali uzazi wa mpango