Jumuiya ya madola kuwakutanisha mawaziri wa sheria Z’bar

NA MWANDISHI MAALUM

TANZANIA inatarajai kuwa mwenyeji wa mkutano wa mawaziri wa sheria wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola, utakaofanyika visiwani Zanzibar kuanzia Machi 4 hadi mwaka huu.

Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Pindi Chana, alieleza hayo jana katika ukumbi wa Idara ya Habari wa Bungeni jijini Dodoma, ambapo alisema maandalizi ya mkutano huo wa kimataifa yanaendelea.

Alisema katika mkutano huo, Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya sheria kutoka nchi na mataifa 56 wakiambatana na maofisa waandamizi pamoja na wageni takriban 300 kutoka nchi za jumuiya ya Madola wanatarajiwa kuhudhuria.

Dk. Chana alisema mkutano huo utajadili mifumo ya kisasa ya uvumbuzi wa kiteknolojia na mambo ya kijidijitali yanavyoweza kusaidia kuongeza ufanisi kwenye tasnia ya sheria na utoaji haki.

 

“Katika mkutano huo Tanzania tunawania tuzo mbili moja ni usajili wa watoto chini ya miaka mitano na nyingine ni utoaji wa huduma ya msaada wa kisheria kupitia kampeni ya Mama Samia legal aid campaign”, alisema Waziri huyo.

Mkutano huu sio tu utaiunganisha Tanzania na anga za kimatifa pekee bali, utatumika kama chazo cha mapato ya fedha za kigeni na kwamba mkutano huo utakuwa wa hapa nchini.

Alisema kuwa dunia ina imani na Tanzania kuhusu utawala wa sheria na haki, ndio maana mnamo mwishoni mwa mwaka mkutano mkubwa wa 77 wa haki za binadamu na watu ulifanyika nchini nchini Tanzania katika mkoa wa Arusha.

“Ikumbukwe kuwa Kamisheni ya Afrika ya haki za binadamu na watu hawaendi mahali bila kujihakikishia masuala ya amani hayapo vizuri, hivyo niwasihi wanahabari kuendeleza kuzitumia kalamu zenu katika kueneza tunu ya amani na mazuri yote ambayo serikali inayatekeleza”, alisema.

Balozi Chana alisema kufanyika mkutano huo kunadhihirisha pasi na shaka juu ya kuaminika kwa Tanzania katika anga la kimataifa kwani mkutano wa mwisho wa mawaziri wa jumuiya ya Madola ulifanyika Mauritius mwaka 2022.

Alisema kwa kawaida sio rahisi mkutano unaofuata kufanyika tena Afrika ila kwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassansita ameifungua nchi na hatimaye kukubaliwa bila kupingwa kuwa mwenyeji wa mkutano huo.

Katika mkutano huo anatarajiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan kufungua na  mkutano huo kufungwa na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi.

 

Comments

Popular posts from this blog

ZALIRI, FLI zaingia makubaliano kuimariusha sekta mifugo

Ibueni changamoto zinazokamisha usawa wa kijinsia - Simbaya

Uislam unakubali uzazi wa mpango