NBC yazindua kampeni ya ‘Shinda Mechi Zako Kinamna Yako’ kukuza uchumi wa wateja wake

BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua kampeni mpya ya akiba inayolenga kuunga mkono juhudi za serikali za kuchochea ukuaji wa uchumi kupitia huduma za kidigitali zinazotolewa na taasisi za kifedha nchini. Kampeni hiyo ya ‘Shinda Mechi Zako Kinamna Yako’ inawahusu wateja binafsi, waajiriwa, wamiliki wa biashara ndogo na wanafunzi ambayo itaambatana na zawadi mbali mbali ikiwemo ya gari mbili aina ya BMW x1. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo jijini Dar es salaam jana, Mkuu wa kitengo cha masoko wa benki hiyo, David Raymond, alieleza kuwa mpango huo unalenga kuimarisha ustawi wa kifedha miongoni mwa wateja wa benki hiyo na kuchochea ukuaji wa uchumi jumuishi kupitia huduma rasmi za kifedha. “Tunanalenga kuitumia falsafa ya mchezo wa soka ambao benki ya NBC ni Wadhamini wakuu wa ligi tatu. Tunapoingiza falsafa hiyo kwenye maisha ni wazi tunatambua wateja wetu wana ndoto, malengo na maazimio katika kufanikisha maendeleo yao kiuchumi yakiwemo ya ujenzi, kukuza bia...