NBC yazindua kampeni ya ‘Shinda Mechi Zako Kinamna Yako’ kukuza uchumi wa wateja wake
BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua kampeni mpya ya akiba inayolenga kuunga mkono juhudi za serikali za kuchochea ukuaji wa uchumi kupitia huduma za kidigitali zinazotolewa na taasisi za kifedha nchini.
Kampeni hiyo ya ‘Shinda
Mechi Zako Kinamna Yako’ inawahusu wateja binafsi, waajiriwa, wamiliki wa
biashara ndogo na wanafunzi ambayo itaambatana na zawadi mbali mbali ikiwemo ya gari mbili aina
ya BMW x1.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo jijini Dar es salaam jana, Mkuu wa kitengo cha masoko wa benki hiyo, David Raymond, alieleza kuwa mpango huo unalenga kuimarisha ustawi wa kifedha miongoni mwa wateja wa benki hiyo na kuchochea ukuaji wa uchumi jumuishi kupitia huduma rasmi za kifedha.
“Tunanalenga kuitumia falsafa ya mchezo wa
soka ambao benki ya NBC ni Wadhamini wakuu wa ligi tatu. Tunapoingiza falsafa
hiyo kwenye maisha ni wazi tunatambua wateja wetu wana ndoto, malengo na
maazimio katika kufanikisha maendeleo yao kiuchumi yakiwemo ya ujenzi, kukuza
biashara, kusomesha watoto na mengine mengi”, aalieleza Raymond.
Aliongeza kuwa mkakati
huo unahusisha agenda ya kutoa elimu kwa wananchi na kuwashawishi watumie
huduma rasmi za kibenki zinazogusa rika na makundi yote ya kijamii na kutaja
huduma zinazohusishwa na kampeni hiyo kuwa ni pamoja na akaunti ya Chanua
ambayo ni mahususi kwa watoto, Malengo, Akaunti ya Johari mahususi kwa wanawake
na akaunti ya Mwalimu.
Alitaja akaunti nyengine
kuwa ni ya mshahara, akauti ya wajasiriamali, akaunti ya wanafunzi, akaunti ya
kua nasi, akaunti ya vikundi, akaunti binafsi na akaunti ya biashara.
Akizungumzia zawadi
zinazotolewa kupitia kampeni hiyo, Meneja Bidhaa na Mauzo, Dorothea Mabonye, alisema
itadumu kwa mwaka mmoja inahusisha zawadi za kila mwezi na mwisho wa mwaka
ikiwemo zawadi kuu ya gari aina BMW X1.
Alieleza kuwa zawadi
hizo zitakazotolewa kwa washindi wawili, fedha taslimu, zawadi ya safari ya
mapumziko nchini Singapore, simu za mikononi, komyuta mpakato (laptops), friji,
‘tablets’ za watoto pamoja na majiko ya kisasa ya kupikia.
Mmoja wa mabalozi
wa kampeni hiyo, Nasry Ramadhani ‘Ujugu’ ambae ni mjasiriamali aliyewekeza
kwenye biashara ya kuonesha burudani ya mpira kupitia TV jijini Dar es salaam, aliwasihi
wajasiriamali wakiwemo vijana kutumia vema fursa hiyo iliyotolewa na benki ya
NBC kupitia kampeni hiyo ili waweze kunufaika kupitia faida mbalimbali
zitokanazo na matumizi ya huduma rasmi za kifedha.
Comments
Post a Comment