Dk. Samia akemea viongozi wachonganishi

NA MWANDISHI MAALUM, MUNDULI

RAIS   wa   Jamhuri   ya   Muungano   wa   Tanzania,   Dk.   Samia   Suluhu   Hassan ameeleza kusikitishwa kwake na baadhi ya viongozi wasiotambua dhamana walizonazo wanaotumia   nafasi   zao   kuchonganisha serikali na jamii badala  ya   kuleta  maelewano.

Rais Samia amesema hayo, wakati akizungumza katika Kumbukumbu ya Miaka 40 ya kifo cha Hayati Edward Moringe Sokoine huku akiwasisitiza viongozi kuiga mfano  wa Sokoine kwani alikemea jambo hilo kwa maneno na vitendo.

Rais   Samia   amesema   Hayati Sokoine   alitumia   utashi   wake   wa   hali   ya   juu kuimarisha   mahusiano   kati   ya   serikali   na   jamii   aliyoiongoza   na   kuiwakilisha vyema jamii ya Wamaasai.

Aidha amewataka   viongozi   wa   sasa   na   wajao  kutambua   kuwa   uamuzi ukifanyika ndani ya serikali ni wajibu wao kuutekeleza kama ulivyo hata ikibidi wao wawe mfano kwa wengine kama Hayati Sokoine alivyofanya.

Kuhusu   umuhimu   wa   elimu   kama  ulivyopewa   kipaumbele  na   Hayati  Sokoine, Rais Samia ametoa wito kwa wazazi kutumia vyema fursa ya miundombinu bora ya Elimu inayojengwa na serikali kuwapeleka watoto shule.

Aidha Rais Samia ametoa wito kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi   wa   Umma   na   Utawala   Bora,   kuendelea   kutunza   kumbukumbu   za viongozi wa kitaifa na kuhakikisha habari zao zinawafikia vijana wengi zaidi kupitia njia za kisasa.

Rais   Samia   ametumia   fursa   hiyo   pia   kutoa   pole   kwa   waathiriwa   wote   wa mafuriko   na   kuahidi   kuwa   serikali   itaendelea   kufanya   kila   linalowezekana kuepusha   madhara   zaidi   na   kuwataka   pia   wananchi   kusikiliza   maelekezo   ya tahadhari zinazotolewa.

Pia   Rais   Samia   amesema   baada   ya   mvua   hizo   na   hali   ya   kawaida   kurejea, Serikali itafanya uchunguzi wa kina kubaini sababu za mafuriko hayo ili kuepusha madhara makubwa kwa siku zijazo.

Comments

Popular posts from this blog

ZALIRI, FLI zaingia makubaliano kuimariusha sekta mifugo

Ibueni changamoto zinazokamisha usawa wa kijinsia - Simbaya

Uislam unakubali uzazi wa mpango