Mfumo kidigitali anuani za makaazi wazinduliwa

NA SAIDA ISSA, DODOMA

SERIKALI kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Wizara ya nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI imezindua majaribio ya kutoa huduma ya barua ya utambulisho wa mkazi kupitia mfumo wa kidijitali wa anwani za makazi (NaPA).

Hatua hiyo ilienda sambamba na kutoa vitendea kazi kwa watendaji wa Kata na Shehia zitakazofanyiwa majaribio kwa Tanzania bara na Zanzibar.

Uzinduzi huo umefanyika jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mohamed Khamis Abdullah (pichani) aliyesema mfumo wa anuani za makazi umetengenezwa kwa dhumuni la kimarisha utoaji wa huduma ndani ya serikali na sekta binafsi ili kuiwezesha nchi kunufaika na fursa za uchumi wa kidijitali na kuimarisha masuala ya utambuzi na usalama ndani ya nchi.

Aidha alisema kuwa ‘operesheni anuani za makazi’ ilikuwa na mafanikio ambapo zaidi ya anuani za makazi milioni 12.3 zilisajiliwa na taarifa zake kuhifadhiwa kwenye mfumo anuani za makaazi wa taifa (NaPA).

KATIBU Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mohamed Khamis  Abdullah(kulia)akimkabidhi Mkurugenzi Msaidizi, Divisheni ya Uendelezaji Miji na Vijiji, Rachel Kaduma,sehemu ya vitendea kazi vitakavyotuMIka katika mfumo wa kitaifa wa kidijitali wa anuani za makazi (NaPA). 

Aidha alisisitiza kuwa usalama wa eneo la mtu anapoishi unaanzia kwa kutambua majirani zake hivyo alihimiza wananchi kuzitumia kwa kuwa sasa dunia imejikita katika utoaji wa huduma kwa mfumo wa kidijitali.

"Kimsingi huduma hii inakwenda kufanyika katika maeneo yetu ya ngazi za msingi ya kata, mitaa na vijiji ambayo tunayasimamia,hivyo Ofisi ya Rais – TAMISEMI italisimamia suala hili kikamilifu na kwa kiwango kikubwa sana kama ilivyotarajiwa", alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Divisheni ya Uendelezaji Miji na Vijiji, Rachel Kaduma, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, alisisitiza kuwa moduli ya utoaji wa barua ya utambulisho kidijitali OR - TAMISEMI italisimamia kimamilifu na kwa kiwango kikubwa kama ilivyotarajiwa pamoja na kuhakikisha kila mtu anatimiza wajibu wake ili matarajio ya serikali yaweze kufikiwa.

Vile vile Kaduma alieleza kuwa hatua hii ni utekelezaji wa zile ‘R’ nne za Dk. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hususani ile ya ‘Reforms’ maana kupitia huduma hii tutakwenda kuleta mageuzi katika utoaji wa huduma kwa kutoa barua ya utambulisho pasipo kufika ofisi za ngazi za msingi”, alieleza Kaduma.

Alifafanua kuwa kwa lugha rahisi ‘NaPA’ ni daftari la kidijitali la ukazi lilonawezesha serikali kuu, serikali za mtaa/kata au shehia ambapo pamoja na mambo mengine kuwejua idadi wa watu walio kwenye eneo husika hivyo urahisi wa kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo kwa kuzingatia uhalisia wa watu na huduma zilizopo katika eneo hilo.

Comments

Popular posts from this blog

ZALIRI, FLI zaingia makubaliano kuimariusha sekta mifugo

Ibueni changamoto zinazokamisha usawa wa kijinsia - Simbaya

Uislam unakubali uzazi wa mpango