Ujenzi wa ofisi, maabara za ZBS Pemba kukamilika mwaka huu

TAASISI ya Viwango Zanzibar (ZBS) imesema ina mpango wa kutekeleza mradi  wa ujenzi wa ofisi na maabara mbali mbali za kisasa za ukaguzi huko Chamanangwe kisiwani Pemba ili kuongeza ufanisi.

Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo, Yussuph Majid Nassor,  ameyasema hayo wakati akifungua Jukwaa la Vyombo vya Habari lililoandaliwa na taasisi hiyo kwa uratibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) na kufanyika katika ofisi za makao makuu ya taasisi hiyo, Maruhubi wilaya ya Mjini Unguja.


MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS), Yussuph Majid Nassor, akizungumza wakati wa jukwaa la pili la viwango na vyombo vya habari katika ofisi za taasisi hiyo Maruhubi. Kulia ni Meneja Uhusiano na Masoko wa taasisi hiyo Aisha Abdulkheir na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC), Tabia Makame Mohammed. 

Amesema hatua hiyo imelenga kuongeza ufanisi wa taasisi hiyo kwenye ukaguzi, udhibiti na uthibitishaji wa viwango vya bidhaa zinazozalishwa na kuingizwa nchini kwa manufaa ya wananchi na mazingira.

Ameongeza kuwa kufanya hivyo pia kutapunguza changamoto ya kusafirisha sampuli za bidhaa kuja Unguka kwa ajili ya uchunguzi hivyo kupunguza muda wa kusubiri majibu ambapo jumla ya shilingi Bilioni 6.5 zinatarajiwa kutumika.

“Tayari zabuni za ujenzi zimeshatangazwa baada ya kukamilika kwa hatua za awali za ujenzi huo ikiwemo ya usanifu wa michoro na ujenzi utakapoanza utachukua miezi 24 hadi kukamilika kwake hivyo kupanua wigo wa utendaji”, ameeleza Majid.

Akizungumzia uimarishaji wa majukumu ya taasisi hiyo, Majid ameeleza kuwa imeendelea kuimarisha maabara za taasisi hiyo zilizozinfduliwa mwaka uliopita pamoja na kukamilisha hatua za awali za kituo cha ukaguzi wa magari kitakachofunguliwa baadae mwezi huu. 

Waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali wakiwa katika jukwaa la pili la viwango na vyombo vya habari.

Amesema pia wana mradi wa kituo cha magari umegharimu shilingi bilioni 2.5 umekamilika katika hatua ya majengo ambapo wiki ijayo kazi ya ufungaji mitambo inatarajiwa kuanza hivi punde.

“Wiki ijayo kazi ya ufungaji wa mitambo ya kituo hicho cha kisasa cha ukaguzi wa magari na vyombo vya moto kielektroniki itaanza na ndani ya mwezi mmoja na nusu ya kituo hicho kitakuwa tayari hivyo tunatarajia mnamo mwezi Juni kitafunguliwa rasmi”, ameeleza Mkurugenzi huyo.

Mbali na miradi ya ujenzi, majid alieleza kuwa taasisi hiyo mimepata mafanikio kadhaa yakiwemo ya kutambuliwa kimataifa na shirika la viwango ulimwengini na baadhi ya maabara zake kupata alama ya ithibati ubora ya mashirika ya kikanda likiwemo la ukanda wa Kusini mwa Afrika.

Aidha amepongeza mashirikiano yanayotolewa na vyomvo vya Habari kupitia ZPC na kuahidi kuuendeleza ili kuipasha habari jamii huku akieleza kuwa ZBS ipo tayari kushirikiana na waandishi wa habari.


AFISA Maabara ya ujenzi katika Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS), Salim Kassim Juma, akitoa maelezo kwa waandishi wa habari juu ya vifaa vya maabara hiyo vinavyotarajiwa kufungwa hivi karibuni. 

Akizungumza katika jukwa hilo, Makamu Mwenyekiti wa ZPC, Tabia Makame Mohammed, ameeleza kufurahishwa kwake na jinsi taasisi hiyo inavyofungamana na vyombo vya habari na kuomba taasisi nyengine kuiga mfano huo.

Ameeleza kuwa vyombo vya Habari ni daraja linanowakutanisha wananchi na taasisi za umma au binafsi hivyo  wanpaswa kufanya kazi kwa pamona na mashirikiano ya hali ya juu.

Aidha aliipongeza kwa kuendelea kupiga hartua za maendeleo ikiwemo ya kujitegemea kwa asilimia 100 hivyo kuiondolea mzigo wa uendeshaji jambo linalotokana na usimamizi bora wa ukusanyaji wa mapato na utoaji wa huduma bora.

Katika jukwaa hilo linalofanyika kwa mara ya pili, waandishi wa habari zaidi ya 50 kutoka vyombo mbali mbali vya habari walishiriki ambapo mada kuhusu uanzishwaji wa maabara ya metrolojia na ushajihishaji na uthibitishaji wa alama ya ubora ziliwasilishwa na kujadiliwa.

Comments

Popular posts from this blog

ZALIRI, FLI zaingia makubaliano kuimariusha sekta mifugo

Ibueni changamoto zinazokamisha usawa wa kijinsia - Simbaya

Uislam unakubali uzazi wa mpango