Dk. Samia aweka maneno ushindi wa Stars AFCON

MUDA mchache baada ya kumalizika kwa mchezo kati ya timu ya taifa ya tanzania ‘TAifa Stars’ na Guinea, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amewapongeza wachezaji, viongozi na watanzania kwa timu hiyo kuibuka na ushindi wa goli 1 – 0.

Kupitia kupitia mtandao wa kijamii wa X (zamani Twitter), Dk. Samia alieleza;  “Tukiwa katika majonzi na kazi ikiendelea katika kuwatafuta ndugu zetu ambao tunaamini bado wapo hai kufuatia kuporomoka kwa jengo eneo la Kariakoo, ninawapongeza vijana wetu Taifa Stars kwa ushindi na kufuzu kushiriki Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025”.

Dk. Samia aliongeza kwa kusema; “Mmeandika historia kwa Taifa letu, ikiwa ni mara yetu ya nne kufikia mafanikio haya makubwa katika kipindi cha zaidi ya miaka arobaini”.

Alliongeza kwa kusema; “Hongera kwa kazi nzuri nyote tuliowapa dhamana kusimama na vijana wetu kukamilisha jukumu hili katika Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), Benchi la Ufundi na Watanzania wote kwa kuendelea kuipenda, kuithamini na kuipa hamasa Timu ya Taifa”.Aidha Dk. Samia alieleza kuwa; “Baada ya ushindi huo, sasa tujikite katika maandalizi mazuri zaidi kwa mashindano yajayo”. 

Taifa stars iliyokuwa ikiwania kufuzu kucheza michuano hiyo, iliibuka na ushindi kufuatia bao lililofungwa mshambuliaji Simon Msuva mnamo dakika ya 61 na kumfanya nyota huyo kuwa na jumla ya magoli 24 aliyoyafunga akiwa na timu za taifa.

Mchezo huo umechezwa Majira ya saa 10:00 jioni kwenye dimba la Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam, kabla ya kuanza timu zote zilisimama kwa dakika moja kutoa heshima kwa watu waliofariki katika ajali ya kuanguka kwa jengo la ghorofa katika mitaa ya Kariakoo, jijini Dar es salam hivi karibuni.



Aidha Rais Samia aliwapongeza vijana hao na watu wote waliopewa dhamana ya kusimama na vijana  timu hiyo kwa kukamilisha jukumu hilo ikiwemo Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), Benchi la Ufundi na Watanzania kwa ujumla.


Comments

Popular posts from this blog

ZAMECO yakerwa na video ya udhalilishaji mtandaoni

Airtel Foundation yazindua mpango wa udhamini wa masomo kwa vijana

SMZ yawaita vijana kushiriki kilimo