Dk. Samia ainua hali za wakulima wa korosho Lindi

 NA MWANDISHI WETU

IMEELEZWA kuwa hatua ya Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kupandisha bei ya korosho ni miongoni mwa ahadi alizozitoa kuimarisha maisha ya wakulima kwa kuwapatia bei nzuri ya mazao yao.

Akizungumza wakati wa mnada wa 10 wa zao hilo, Ofisa usimamizi wa fedha wa Soko la Bidhaa Tanzania(TMX), Prince Mng'ong'o, alieleza kuwa hali hiyo inakwenda sambamba na kuongeza ununuzi wa zao hilo lililofikia tani 401,000 zenye thamani ya shilingi Trilioni 1.44 kwa mwaka 2024/2025.

Alieleza kuwa mafanikio hayo ni pamoja na kupandishwa kwa bei ya zao hilo, yameongeza thamani kwa mkulima na kupandisha uchumi wa Taifa ambapo wakati msimu wa ununuzi wa korosho kwa mwaka 2024/2025 ukikaribia kumalizika mpaka sasa kiasi hicho cha tani hizo za Korosho zimenunuliwa.

Katika Mnada wa kumi wa chama Kikuu cha Ushirika cha RUNALI kwa msimu wa 2024/2025 uliofanyika Mjini Nachingwea, Mng'ong'o alisema, hadi sasa kiasi hicho cha tani za korosho ghafi za Trilioni 1.44 zimeuzwa na kununuliwa.

Aidha Mng'ongo alisema hadi sasa chama kikuu cha RUNALI kimefanikiwa kuuza tani 70,360 kati ya tani 401,000 zilizozalishwa na Mikoa yote mitano inayolima zao hilo kwa wingi hapa nchini.

“Mbali na korosho Taasisi hiyo imeweza kusimamia mauzo kupitia minada  ya zao la kakao ambapo hadi sasa takribani tani 11,000 zenye thamani ya Shilingi Bilioni 210 zimeuzwa na kununuliwa”, alieleza Mng’ongo.

Aliongeza kuwa; "Lakini pia TMX imeendesha minada ya madini, mpaka sasa zimeuzwa gramu 610,000 ambazo sawa na kilo 610 zenye thamani ya Shilingi Bilioni 610 kwa njia ya soko la bidhaa Tanzania, mkakati ni kwamba ifikapo mwaka 2025 mazao yote ya kimkakati yauzwe kwa  mfumo wa TMX".


Chama kikuu cha RUNALI kilichopo Mkoani Lindi kinatarajia kufanya mnada mmoja wa mwisho, ambapo baadhi ya Vyama Vikuu vya Ushirika tayari vimefunga msimu wa ununuzi kwa mwaka 2024/2025.

Katika mnada wa kwanza wa Mikoa ya Kusini ya Lindi na Mtwara, Oktoba 11, 2024, Rais Samia alipandisha bei ya korosho na kuuzwa kwa bei ya juu ya Shilingi 4,120 kwa kilogramu, huku bei ya chini ikiwa Shilingi 4,035.

Comments

Popular posts from this blog

ZAMECO yakerwa na video ya udhalilishaji mtandaoni

Airtel Foundation yazindua mpango wa udhamini wa masomo kwa vijana

SMZ yawaita vijana kushiriki kilimo