Dk. Samia amechochea mafanikio michezoni - BMT

NA SAIDA ISSA, DODOMA KATIBU Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Neema Msitha (pichani), ameeleza mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya michezo ndani ya miaka minne, akisisitiza mchango wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, kuhamasisha na kuimarisha mazingira ya michezo nchini. Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dodoma, Msitha alisema kuwa katika kipindi hicho, kumekuwa na ongezeko kubwa la ufadhili, ujenzi wa miundombinu ya kisasa na ushirikiano wa kimataifa, hatua ambazo zimechangia mafanikio makubwa katika sekta ya michezo. Miongoni mwa miradi ya miundombinu iliyotekelezwa ni ukarabati wa Uwanja wa Benjamin Mkapa uliogharimu shilingi bilioni 31, ujenzi wa uwanja mpya wa michezo jijini Arusha wenye gharama ya shilingi bilioni 338, pamoja na ujenzi wa uwanja mpya wa michezo Dodoma utakaogharimu shilingi bilioni 310. "Serikali imewekeza shilingi bilioni 21 katika ujenzi wa viwanja vya mazoezi kama Gymkhana, Leaders Club, TIRDO...