Mtanda aipongeza Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kuwafikishia wananchi huduma

NA MWANDISHI WETU, MWANZA

MKUU wa mkoa wa Mwanza, Saidi Mtanda amezindua Kamati ya Ushauri wa Kisheria ya mkoa huo na Kliniki ya Sheria bila malipo kwa wananchi wa iliyoanza Februari 17 hadi 23, 2025 na kuipongeza ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali kwa kuwafikishia huduma wananchi katika maeneo yao.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kliniki hiyo, Mtanda amempongeza Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari pamoja na Ofisi yake kwa kuuchagua mkoa wa Mwanza na kufanya kliniki hiyo inayotarajiwa kutatua changamoro mbali mbali zinazohusu sheria.

Aidha, Mkuu wa mkoa wa Mwanza, ameeleza kuwa kliniki hiyo ni sehemu ya juhudi za Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kusogeza huduma karibu na wananchi kwa kuwafikia kwenye maeneo yao wanayoishi.

Katika hatua nyingine, Mtanda ametoa wito kwa wananchi kutembelea kwenye viwanja vya kliniki hiyo ili waweze kupatiwa ufumbuzi wa changamoto mbali mbali za kisheria zinazowak“Niwaombe wananchi kutumia fursa hii, mje mpate huduma za kisheria kutoka kwa Mawakili wetu, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeona itekeleze maono ya Mhe. Rais ya kuwafikishia huduma za kisheria wananchi ambao hawana uwezo wa kupata huduma hizo”, aliongeza Mtanda.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma za Ushauri na Uratibu wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Neema Ringo, akimuwakilisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali, amesema kuwa Kamati za Ushauri wa Kisheria katika ngazi ya mkoa na wilaya zimeanzishwa kwa lengo la kutatua migogoro mbalimbali ya kisheria baina ya wananchi na Serikali au wananchi kwa wananchi.

“Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imetoa Mwongozo wa kusikiliza wananchi kupitia Kamatii za Ushauri wa Kisheria katika ngazi ya Mikoa na Wilaya”, alieleza Ringo.

Aidha Ringo amesema kuwa uzinduzi wa Kliniki ya Sheria bila malipo kwa wananchi wa Mkoa wa Mwanza ni mojawapo ya hatua za Ofisi yake kusogeza huduma kwa wananchi na kupunguza kesi dhidi ya serikali.

“Tumekuwa tukipokea kesi na mashauri yanayofunguliwa dhidi ya serikali, katika kuhakikisha kuwa suala hilo tunalitatua tuliona tuje na utaratibu huu wa Kiliniki ya Sheria ili tuweze kushughulikia masuala mbalimbali ya kisheria”, alieleza Ringo.

Comments

Popular posts from this blog

ZAMECO yakerwa na video ya udhalilishaji mtandaoni

Airtel Foundation yazindua mpango wa udhamini wa masomo kwa vijana

SMZ yawaita vijana kushiriki kilimo