PUMA ENERGY YAJIDHATITI KUFANYA KAZI NA WADAU SEKTA YA ANGA ZANZIBAR

NA MWANDISHI WETU

KAMPUNI ya Puma Energy Tanzania  imeeleza kuwa itandelea kufanya kazi kwa karibu na wadau wa sekta ya usafirishaji wa anga ili kukuza kasi ya biashara na uchumi wa Zanzibar.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Fatma Abdallah, amesema hayo wakati wa futari maalum iliyowakutanisha viongozi wa dini, serikali na wadau wakuu wa sekta ya nga katika jioni ya shukrani, mshikamano na tafakari katika mwezi mtukufu wa Ramadhani iiyofanyika hoteli ya Golden Tulip, Uwanja wa ndege, Zanzibar.

Ameeleza kuwa lengo la futari hiyo ni kuimarisha umoja kwani ushirikiano uliopo sasa umesaidia kufanikisha biashara ya kampuni hiyo Zanzibar.

"Kama yalivyo matumaini ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar pia nasi tuna matarajio makubwa ya kutanua huduma muhimu zitakazowafikia wananchi kupitia miradi ya uwekezaji inayoanzishwa nchini”, ameeleza Fatma.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar (ZAA), Seif Abdallah Juma (wa pili kushoto), amesema lengo la kuwepo miradi hiyo ni kukuza sekta ya huduma na biashara ili kukuza pato la nchi.

Seif ameeleza kuwa kuimarika kwa huduma za sekta ya anga Zanzibar kumeongeza mvuto kwa mashirika makubwa ya usafirishaji wa anga ulimwenguni na kuamua kuwekeza na kutoa huduma katika viwanja vya ndege vya Zanzibar jambo ambalo pia limerahisisha usafiri na usafirishaji wa abiria na mizigo.








KaKa

K






Hivyo amesema wataendelea kushirikiana na wadau kama Puma Energy kuimarisha sekta za biashara na utalii ambazo ni uti wa mgongo wa uchumi wa Zanzibar na kuiomba Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji Zanzibar (ZURA) kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za mafuta ya ndege na mitambo inayofikia viwango vya kimataifa.

Kampuni ya Puma Energy Tanzania ni wauzaji wa aina mbali mbali za mafuta ya vyombo vya moto na vilainishi imekuwepo Zanzibar tangu mwaka 1994 wakati huo ikijulikana kama BP Tanzania.

Comments

Popular posts from this blog

ZAMECO yakerwa na video ya udhalilishaji mtandaoni

Airtel Foundation yazindua mpango wa udhamini wa masomo kwa vijana

SMZ yawaita vijana kushiriki kilimo