IPA tanuri la kuimarisha utumishi wa umma Z'bar

NA MWANAJUMA SAID, IPA KATIKA kuimarisha mifumo ya utoaji huduma serikalini, hakuna jambo muhimu kama kuwa na watumishi wa umma wenye uwezo, maarifa na maadili ya kazi. WAZIRI wa Nchi (AR) Katiba, Sheria,Utumishi na Utawala Bora , Dk. Haroun Ali Suleiman , akizungumza na uongozi wa Chuo cha Serikali cha Kenya waliofika ofisini kwake Mazizini kwa ajili ya kujitambulisha. Kwa kuliona hilo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kupitia Chuo cha Utawala wa Umma Zanzibar (IPA) imeendelea kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha nguvu kazi ya taifa inaimarishwa kupitia mafunzo ya kitaaluma na kiutendaji. Chuo hi ch o ki licho anzishwa kwa sheria n amba moja ya mwaka 2007 ni taasisi ya kiserikali ambayo iko chini ya Wizara ya Nchi , Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala bora. Miongoni mwa majukumu ya c huo hiki ni k utoa mafunzo kwa watumishi wa umma, sekta binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali kwa lengo la kuongeza ufanisi, uwajibi...