ZiBi, OER waiweka Zanzibar kwenye ramani ya uwekezaji duniani

NA MWANDISHI WETU

JARIDA la Biashara na Uwekezaji Zanzibar (Zanzibar Investment and Business Insights  -ZiBi) limeweka historia baada ya kutambulika rasmi kama mshirika wa kimataifa wa jarida  maarufu la biashara katika nchi za Ghuba la Oman Economic Review (OER).

Taarifa iliyotolewa na waandaaji wa jarida hilo, ilieleza kuwa hatua iliyofikiwa ni kubwa kwa sekta binafsi ya Zanzibar na uthibitisho wa uwezo wa taasisi za ndani kushindana na kushirikiana kimataifa.

Katika kilele cha Oman Economic Review Business Summit 2025 iliyofanyika Aprili 30, 2025 mjini Muscat, ZiBi ilialikwa kama Mgeni Maalum na kutangazwa kuwa ni Msirika wa habari kwa Zanzibar (Media Partner – Zanzibar) huku ikiwakilishwa na Mjumbe wa Bodi ya ZiBI, Masoud Salim.

“Wakati wa hafla hiyo, ZiBi ilitunukiwa tuzo maalum ya kutambuliwa kama mshirika wa habari kutoka Zanzibar ikia ni ishara ya heshima kubwa kwa mchango wake katika kukuza uhusiano wa kiuchumi kupitia taarifa, uchambuzi na uandishi wa kimaendeleo”, ilieleza taarifa hiyo.

Mjumbe wa Bodi ya ZiBI, Masoud Salim (katikati) akipokea tunzo maalum baada ya kutangazwa kuwa ni Mshirika wa habari (Media Partner – Zanzibar) wa jarida la Oman Economic Review (OER).  

Makubaliano ya ushirikiano yalitiwa saini hivi karibuni kati ya Oman Economic Review na kampuni ya Mwanana Communications Co. Ltd (wachapishaji wa ZiBi), yanakusudia kubadilishana makala kuhusu fursa za kibiashara, kuandaa matukio ya pamoja ya kibiashara Zanzibar na Oman na kuratibu misafara ya wafanyabiashara kati ya nchi hizi mbili.

“Tunaiona ZiBi kama sauti ya Zanzibar katika masuala ya maendeleo na biashara. Ushirikiano huu ni hatua ya kujivunia na unafungua milango mipya kwa Zanzibar kutambulika kimataifa”, alisema Prof. Mohamed Hafidh Khalfan, Mwenyekiti wa Bodi ya ZiBi.

WAZI wa nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Shariff Ali Shariff (wa pili kushoto)  akizungumza wakati wa uzinduzi wa tolea oa tatu la Jarida la Biashara na Uwekezaji Zanzibar (ZiBi) uliofanyika hoteli ya Verde, Zanzibar.

Kwa upande wake, Mhariri Mtendaji wa jarida hilo, Hissham Abdulkadir, alieleza; “Tunajivunia ushirikiano huu na jarida kongwe kama Oman Economic Review. Kupitia makala, mijadala na matukio ya pamoja, tutaupeleka ujumbe wa Zanzibar mbali zaidi, hasa kwa wawekezaji wa nchi za Ghuba”.

Aliongeza kuwa jarida la ZiBi si geni nchini Oman ambapo mwaka 2024 jarida hilo lilishiriki kwenye Jukwaa la Biashara la Tanzania na Oman na kuchapisha makala maalum kuhusu kongamano hilo. 

Comments

Popular posts from this blog

Airtel Foundation yazindua mpango wa udhamini wa masomo kwa vijana

ZAMECO yakerwa na video ya udhalilishaji mtandaoni

SMZ yawaita vijana kushiriki kilimo