https://youtu.be/kWQIDmIAFkQ
ZAMECO yakerwa na video ya udhalilishaji mtandaoni
NA MWANDISHI WETU KAMATI ya Wataalamu wa Masuala ya Habari Zanzibar (ZAMECO) inayoundwa na taasisi za kihabari na wadau wa habari imelaani video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii inayoonesha wasichana wawili waliorekodiwa na kuulizwa maswali yasiyo na maadili, kuvunja heshima na kukiuka haki za binaadamu. Taarifa iliyotolewa na taasisi hizo na kutiwa saini kwa pamoja na mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC), Abdallah Mfaume na Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA ZNZ), Dk. Mzuri Issa, ilieleza kuwa tukio hili limeibua hisia kali kwa wadau wa habari, watetezi wa haki za binaadamu najamii kwa ujumla. Ilielezwa kuwa tukio hilo pia limeibua maswali yasiyo na majibu miongoni mwa wanahabari kuhusu maadili, haki za binadamu, na misingi ya uhuru wa vyombo vya habari. “Hivyo basi ZAMECO inasisitiza kuwa vitendo vya udhalilishaji kwa watoto wa kike na jamii ni ukiukwaji wa haki za binaadamu, maadili ya uandishi wa habari na kuvuruga ...
Comments
Post a Comment