Kagere aiongoza Simba ikiiadhibu Chipukizi Mapinduzi Cup

NA MWANDISHI WETU

WAWAKILISHI wa Tanzania katika ligi ya mabingwa Afrika Simba SC imeanza michuano ya kombe la mapinduzi kwa ushindi wa mabao 3 – 1 dhidi ya chipukizi FC

Katika mchezo uliopigwa jana majira ya saa 10:00 jioni kwenye uwanja wa Amaan zanzibar, simba ilikutana na ushindani mkali katika kipindi cha kwanza huku wachezaji nwake wakipoteza nafasi nyingi za kufunga.

Ikichezesha sehemu kubwa ya wachezaji wa kikosi cha pili, Simba ilijikuta ikipachikwa bao katika dakia ya 35 lililofungwa na Faki Mwalimu Sharif na kuongeza hamasa ya wachezaji wa hiyo yenye makao makuu yake kisiwani Pemba.

Mchezo huo uliohudhuriwa pia na Makamu wa kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad aliekuwa mgeni rasmi, Simba ilisawazisha bao hilo katika dakika ya 44 kupitia kwa mshambuliaji Medie Kagere kwa njia ya kichwa na kuongeza kasi ya mchezo huku timu hizo zikishambuliana kwa zamu na kupelekea kumaliza dakika 45 za kwana timu hizo zikiwa 1 – 1.

Katika kipindi cha pili timu hizo ziliendelea kushambuliana kwa zamu hadi katika dakiak ya 51 Miraji Athuman alipoipatia bao timu ya Simba kupitia kwa Medie Kagere kabla ya Miraji Athuman kuongeza bao la tatu katika dakika ya 82 na kuwafanya mashabiki wa simba kupiga kidedea.

Kwa matokeo hayo timu ya Chipukizi imeaga mashindano hayo baada ya awali kupoteza mchezo dhidi ya Mtibwa ambapo leo Jamhuri iliyota sare na Yanga katika mchezo wa awali itashuka dimbani kuwakabili wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kombe la shirikisho la soka afrika Namungo FC majira ya saa 10:00 jioni wakati majira ya usiku Simba SC itashuka dimbani tena kuwakabili mabingwa watetezi Mtibwa.

Comments

Popular posts from this blog

ZALIRI, FLI zaingia makubaliano kuimariusha sekta mifugo

Ibueni changamoto zinazokamisha usawa wa kijinsia - Simbaya

Uislam unakubali uzazi wa mpango