
Sandra Nankomah, Lily Kadima kushiriki ‘Mashariki Music Festival’ NA MWANDISHI WETU WASANII Sandra Nankomah na Lily Kadima kutoka Uganda wametajwa kuwa ni miongoni mwa wasanii watakaoshiriki tamasha la muziki la ‘Mashariki Festival’, linalotarajiwa kufanyika Zanzibar baadae mwezi ujao. Akizungumza na waandishi wa habari, Mratibu wa tamasha hilo, John Kagaruki,alieleza kuwa tamasha hilo linafanyika kwa lengo la kupata fedha ziitakazosaidia maendeleo ya Chuo cha Muziki cha Nchi za Majahazi (DCMA). Mratibu wa tamasha 'Mashariki Music Festival' John Kagaruki (katikati) akiwa na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya CPS Ltd, Tobias Dietzold (kushoto) na mtendaji wa chuo cha DCMA, Halda Alkanaan. Kagaruki alieleza kuwa, pamoja na wasanii hao, pia wasanii kutoka Kenya, Tanzania bara na Zanzibar wakiwemo wahitimu wa chuo hicho watafanya maonesho ya muziki na kazi nyengine za sanaa. Aliwataja wasanii na vikundi vitakavyotumbuiza kuwa ni Fadhilee Itulya na Makadem kutoka Kenya, Msafiri Zaw...