GeSCI kuzindua mpango kuimarisha elimu Tanzania

NA MWANDISHI MAALUM

MPANGO kutathmini utungaji na utekelezaji wa sera za elimu nchini Tanzania unatarajiwa kuzinduliwa Machi 24, 2022 katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort Zanzibar.

Taarifa iliyotolewa na taasisi ya Global e-Schools and Communities Initiative (GeSCI), ameeleza kuwa mpango huo unaotekelezwa na chuo kikuu cha Makerere, Uganda na Kituo cha Kimataifa cha Chuo Kikuu cha Notre Dame, umelenga kufanya tafiti, tathmini na kutafsiri sera za ufundishaji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa kupitia mpango wa Tathmini ya Kurekebisha sera za kufundishia (ADAPT), utafiti unafanyika ili kufikia malengo ya kutoa mafunzo kitaifa na kikanda ili kuimarisha maamuzi ya kitaifa yanayotokana na takwimu.

Katika uzinduzi huo, miongoni mwa wageni watakaohudhuria na kuwasilisha taarifa na mada ni pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Tanzania Bara Prof. Eliamini Sedoyeka, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Zanzibar Ali Khamis Juma na Khamis Abdulla Said, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar.

Wengine ni Mkurugenzi Taasisi ya Elimu Zanzibar (ZIE), Abdalla Mussa, Dk. Fika Mwakabungu, Mkurugenzi Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE), Dk. Said Juma, Mkuu wa kitivo cha elimu katika chuo kikuu cha taifa Zanzibar (SUZA) na Khadija Shariff kutoka Milele Zanzibar Foundation.

Wazungumzaji wengine ni Mwanaidi Ali, Mkurugenzi Mtendaji, taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), Sr. Grace Mkosamali, RELI TZ nchi /AMUCTA na Mkurugenzi Mtendaji, UWEZO Tanzania, Zaida Mgalla.

Comments

Popular posts from this blog

ZALIRI, FLI zaingia makubaliano kuimariusha sekta mifugo

Ibueni changamoto zinazokamisha usawa wa kijinsia - Simbaya

Uislam unakubali uzazi wa mpango