Majaliwa: Zingatieni weledi, maadili ya vyombo vya habari
LINDI WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ili kuhakikisha wananchi wanapata habari sahihi vyombo vya habari havina budi kufanya kazi kwa k uzingatia maadili na weledi pamoja na kutanguliza uzalendo na maslahi ya taifa. Pia, Waziri Mkuu amesisitiza kwamba Serikali itaendelea k usimamia matumizi ya mitandao ya kijamii ili pamoja na kuongeza upatikanaji wa habari kuwepo na uzingatiaji wa maadili na weledi. “ Ni matarajio yetu kuwa moja ya majukumu yenu ni kulisemea Taifa letu.” Ameyasema hayo Aprili 14, 2022 wakati akizindua vituo vya kurushia matangazo ya redio vya Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) wilayani Ruangwa, mkoani Lindi kwa niaba ya vituo vingine vya wilaya za Ludewa (Njombe), Mlimba (Morogoro) na Ngara (Kagera). Amesema SERIKALI itahakikisha uhuru wa vyombo vya habari nchini unaimarishwa na kulindwa hivyo wamiliki na wanahabari wanatakiwa kuzingatia maadili ya kazi zao ili wananchi waendelee kupata taarifa sahihi, kwa urahisi zaidi ...