'Andikeni habari zitakazochochea maendeleo '

NA MWANDISHI WETU WANAHABARI nchini wametakiwa kubadilika na kuandika habari zitakazochochea maendeleo ya nchi na watu wake. Wito huo Umetolewa na Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Zanzibar, Hassan Khatib Hassan, (wa katitaki pichani) alipokua akifungua mafunzo ya waandishi wa vyombo mbali mbali vya habari yaliyoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) kwa kushirikiana na shirika la Internews Tanzania, yaliyofanyika katika ukumbi wa Uhuru, Kariakoo Zanzibar. Alieleza kuwa vyombo vya habari ni muhimu kwani vinaweza kuandika habari zenye kuibua hamasa ya wananchi kufikia dhamira ya serikali na kufichua maovu dhidi ya maendeleo ya nchi na watu wake. Hassan aliongeza kuwa wananchi walio wengi wanasikiliza na kufuatilia vyombo vya habari wakiamini kuwa watapata taarifa za ukweli na zinazozingatia weledi na sio taarifa za kubuni ama kughushi. “Iwapo mtajikita zaidi kutaka kuwafurahisha wasomaji na wasikilizaji au watazamaji basi tunaweza kufika pahala tukapote...