Daraja la TASAF lapunguza utoro wa wanafunzi Mjini Wingwi
NA MWANDISHI WETU, PEMBA
WANANCHI wa vijiji vya Chupwe, Sebudawa na Mjini Wingwi wameleeza kuwa ujenzi wa daraja linalounganisha vijiji hivyo umepunguza utoro wa wanafunzi na upatikanaji wa huduma nyengine za jamii.
Akizungumza
na waandishi wa habari waliofika ktika shehia ya Mjini Wingi, wilaya ya Micheweni, mkoa wa Kaskazini Pemba, Mwalimu
dhamana wa skuli hiyo, Juma Khamis Kombo, alisema kabla ya kujengwa kwa daraja
hilo, utoro wa wanafunzi ulikua mkubwa.
Alisema
baada ya kukamilika kwa daraja hilo lililojengwa kupitia miradi ya jamii
ulioibuliwa na wananchi wa shehia hiyo, mahudhurio ya wanafunzi yameimarika.
“Awali
wanafunzi walikuwa wanashindwa kufika skuli kikawaida kutokana na kushindwa
kuvuka kutoka katika makaazi yao na kwenda skuli hasa katika msimu za mvua,”
alieleza mwalimu huyo.
Aliongeza
kuwa awali wananchi walipanga magogo ili kuvuka kutoka eneo moja kwenda jengine
kwa ajili ya shughuli za kijamii wakiwemo wanafunzi ambao walikuwa wakianguka
na madaftari yao kuingia maji.
Alisema
skuli hiyo yenye wanafunzi 1,272 ambapo wanafunzi watoro 118 walirejeshwa skuli
kupitia mradi wa urejeshaji wa wanafunzi skuli unaoendeshwa na Wizara ya Elimu
Zanzibar hapo kabla wastani wa wanafunzi 500 walikua hawahudhuri skuli
kikawaida.
“Wanafunzi
waliorejeshwa tulionao sasa ni wavulana 670 na wasichana 15 ambao walikuwa
wakijihusisha na shughuli mbali mbali zikiwemo za uvuvi na kilimo cha mwani
lakini sasa wapo skuli na baadhi yao tumewafanyia mitihani, wanaendelea vyema,”
alieleza.
Baadhi ya
wananchi wa kijiji hicho, waliipongeza serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya
jamii (TASAF) kwa kuwajengea daraja hilo lenye urefu wa zaidi ya mita 60
linalopita juu ya bwawa la maji bahari linalotenganisha vijiji hivyo.
Aidha
aliiomba serikali kuwajengea daraja la kudumu kutokana na daraja hilo
lililojengwa kwa miti linachakaa hivyo kuwarudisha katika dhiki waliyokuwa
wakiipata awali.
Naye
Mjumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Miradi ya jamii (CMC) katika shehia hiyo,
Masoud Kombo Hassan, alisema awali kabla ya ujenzi wa daraja hilo kulikuwa na
kikwazo kikubwa kwa wananchi hasa wanawake na watoto kuzifikia huduma zikiwemo
za afya au elimu.
Alieleza
kuwa hali hiyo iliwalazimu kupita katika eneo jengine ambalo ni masafa marefu
kufika huduma hizo hali iliyobadilika mwaka mmoja na miezi minne baada ya TASAF
kugharamia ujenzi huo na kuwataka wananchi kulitunza daraja hilo ili kutumika
kwa muda mrefu.
“Tunataka
tufanye harambee kwa ajili ya ujenzi wa daraja la kudumu ili kusaidia kwa
kizazi cha sasa na kinachokuja kwa sababu eneo hili limezungukwa na bahari
hivyo tunahitaji kivuko cha kisasa kilicho bora na cha kudumu,” alisema.
Kaimu
Sheha wa shehia ya Mjini Wingwi, Hussein Makame Hamad, alisema kufunguliwa kwa
daraja hilo kumerudisha furaha ya wananchi wa shehia hiyo na kusisitiza haja ya
kujengwa kwa daraja la kudumu.
Aidha
sheha Hamad, aliwataka watu wenye uwezo na viongozi wa jimbo hilo kusaidia
ujenzi wa kudumu wa daraja hilo na ujenzi wa barabara ili kuimarisha maendeleo
ya kijiji hicho.
Shilingi
milioni 7.3 zimetumika katika ujenzi wa daraja hilo na uimarishaji wa mazingira
ya eneo hilo ambapo zaidi ya miti ya mikoko 3,000 imepandwa na wanufaika wa
mpango wa kunusuru kaya maskini.
Comments
Post a Comment