NMB yaendelea kung'ara benki bora wateja binafsi

NA MWANDISHI WETU

BENKI ya NMB imeshinda tuzo ya benki kiongozi wa kuwahudumia wateja binafsi nchini kutokana na ubora wa huduma zake kukidhi mahitaji ya huduma za kifedha za umma wa walio wengi.

NMB ilitunukiwa tuzo hiyo kwenye hafla ya tuzo za Global Banking and Finance (GBAF) zilizofanyika jijini London, Uingereza zilizoanzishwa mwaka 2011 na jarida la Global Banking & Finance Review lenye wasomaji zaidi ya milioni tatu ulimwenguni kote na ambalo shughuli yake kubwa ni kuangazia matukio na maendeleo ya kifedha duniani kwa mwaka wa pili mfululizo,.

Akizungumza kwenye hafla ya kuwazawadia washindi wa tuzo za mwaka huu, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi, alisema ushindi wa benki hiyo ni kutambuliwa kwa dhamira yake thabiti ya kuwawezesha wateja na kulihudumia kikamilifu taifa kwa ujumla.

“Tunawahudumia wateja binafsi wa aina mbalimbali wakiwemo wakulima wadogo, watumishi wa umma, wafanyakazi wa sekta binafsi na wajasiriamali wa kada zote kuanzia ile ya chini kabisa hadi wale wa kati. Kwenye hilo hatuna mpinzani. Tupo kwa asilimia 100 katika wilaya zote nchini,” Mponzi alisema.

Alieleza kuwa NMB inaongoza kwa kuwa na mtandao mpana wa usambazji huduma wenye matawi 227 ambayo asilimia 70 yake yapo maeneo ya vijijini, na zaidi ya NMB Wakala 15,000 pamoja na zaidi ya mashine za kutolea pesa 750.

“Dira na mkakati wetu wa sasa hivi na siku zijazo ni kuendelea kutumia maendeleo ya teknolojia za kidijitali kutuwezesha kulisukuma gurudumu la huduma jumuishi za kifedha kwa kutoa huduma zinazohimilika, rahisi na zinazofikiwa na wengi kwa wepesi,” alifafanua Mponzi.

Alisema mafanikio iliyonayo NMB yasingewezekana bila mchango na msaada wa Serikali na Benki Kuu ya Tanzania ambazo alisema zimesaidia benki hiyo kustawi na kushamili kwa kuweka mazingira wezeshi na rafiki ya biashara na shughuli za kibenki.

Mponzi pia alibainisha kuwa mipango na ushirikiano wa benki hiyo na wadau wake wote umeiwezesha kuwa na matokeo chanya kwenye jamii na kupelekea kuaminika sokoni. Hali hii imepelekea kukua kwa amana za wateja kwa asilimia 24 hadi TZS trilioni 6.5 mwaka 2021.

 

Comments

Popular posts from this blog

ZALIRI, FLI zaingia makubaliano kuimariusha sekta mifugo

Ibueni changamoto zinazokamisha usawa wa kijinsia - Simbaya

Uislam unakubali uzazi wa mpango