Othman aongoza mazishi ya mke wa mwandishi habari Zanzibar

NA MWANDISHI MAALUM, ZPC

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,  Alhaj  Othman Masoud Othman, Septemba 12, 2022 alijumuika na wananchi na viongozi mbali mbali katika maziko ya mke wa Mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania Daima na mwanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC), Talib Ussi Hamad, bi. Hafsa Said Salum.

Maziko ya bi. Hafsa aliyekua mtumishi wa Baraza la Manispaa Mjini, yalifanyika katika makaburi ya Kianga baada ya kusaliwa katika msikiti wa Weles, mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

Akizungumzia msiba huo uliotokea Septemba 11, mwaka huu, Mwenyekiti wa ZPC, Abdallah Abdulrahman Mfaume, alitoa pole kwa wafiwa na kuwataka kuwa na subira katika kipindi hiki kigumu na kumuombea dua marehemu apumzike kwa amani.

Aidha aliwataka wanachama wa Klabu hiyo na waandishi wa habari Zanzibar kuendeleza umoja na mshikamano kama waliouonesha katika msiba huo kwa kuwa hupunguza machungu na kuongeza faraja kwa wafiwa.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahala Pema, Amin.

Picha na maelezo 

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, akishiriki kubeba jeneza lenye mwili wa marehemu Hafsa Said Salum aliyekua mke wa mwandishi wa habari Talib Ussi Hamad, kabla ya sala maiti iliyofanyika katika msikiti wa Weles, Mjini Unguja.


MWANDISHI wa habari Talib Ussi Hamad, akijumuika na waumini wengine wa dini ya kiislamu wakati wa kisomo cha hitma kwa ajili ya marehemu mkwewe Hafsa Said Salum iliyofanyika katika msikiti wa Weles, Mjini Unguja.

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, akimfariji mwandishi wa habari, Talib Ussi Hamad, baada ya sala maiti iliyofanyika katika msikiti wa Weles, Mjini Unguja.





 


Comments

Popular posts from this blog

ZALIRI, FLI zaingia makubaliano kuimariusha sekta mifugo

Ibueni changamoto zinazokamisha usawa wa kijinsia - Simbaya

Uislam unakubali uzazi wa mpango