SMZ yajidhatiti kusimamia haki, ulinzi wa watoto

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema imejipanga kuimarisha ulinzi na kusimamia upatikanaji wa haki za watoto katika ngazi ya jamii. WAZIRI wa Maendeleo, Jinsia, Wazee, Wanawake na Watoto, Riziki Pembe Juma (pichani), alieleza hayo alipozungumza na mwandishi wa habari hizi wakati wa sherehe maadhimisho ya miaka 77 ya Umoja wa Mataifa (UN) yaliyofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil, Unguja. Amesema hatua hiyo itasaidia kulinda haki, fursa na kuimarisha ustawi na maendeleo hasa katika upatikanaji wa haki za watoto pamoja na kupinga vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto. Amesema mikakati huo utakuwa pamoja na kuwajengea uwezo wa kisheria wanawake ili waweze kulinda na kusimamia haki na mambo mengine ya msingi ya nayo stahiki kupatiwa watoto. Mbali na hilo amesema Wizara hiyo itafanya kazi kwa karibu na Umoja wa Mataifa kwa ...