NA MWANDISHI WETU KAMPUNI ya mawasiliano ya Aiirtel Tanzania imezindua mpango wa udhamini wa masomo katika fani za teknolojia kwa vijana wa Afrika wanaosoma katika taasisi ya teknolojia ya india (IIT – Madras) kampasi ya Zanzibar. Uzinduzi huo umefanyika Oktoba 7, 2024 katika kampasi ya chuo hicho Bweleo, wilaya ya Magharibi ‘B’ Unguja na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Dk. Dinesh Balsingh na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Lela Muhamed Mussa. Viongozi wengine ni Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Omar Kipanga, Balozi wa India nchini Tanzania, Dk. Biswadip Dey, Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Makame Machano Haji na Mkuruaenzi wa IITMZ Prof. Preeti Aghalayam. Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Airtel Africa, Dk. Segun Ogunsanya, Dk. Dinesh amesema programu hiyo inahusisha wanafunzi wa Afrika walofaulu michipuo ya sayansi na kwamba kila mwak...