Vyombo vya habari vinapaswa kusimamia mshikamano wa Afrika - UAJ

NA MWANDISHI MAALUM, CAIRO MSHAURI wa Baraza Kuu la Usimamizi wa Vyombo vya Habari nchini Misri, Reem Hindi, ameeleza haja ya vyombo vya habari barani Afrika kusimamia msingi wa mshikamano wa Kiafrika ili kustawisha maendeleo ya bara na tasnia ya habari kwa ujumla. Alitoa rai hiyo wakati akifungua mafunzo ya 61 yaliyoandaliwa na Umoja wa Waandishi wa Habari wa Afrika (UAJ) kwa kushirikiana na Baraza Kuu la Udhibiti wa Vyombo vya Habari yanayoendelea jijini Cairo, Misri yanayoshirikisha waandishi wa habari kutoka mataifa 20 ya Afrika huku Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) ukiwakilishwa na mwanachama wa Klabu ya Waaandishi wa Habari Zanzibar (ZPC), Khairat Haji Ali. Mshauri huyo aliweka wazi dhamira ya nchi hiyo kuunga mkono jitihada za UAJ za kujenga weledi na uhuru wa vyombo vya habari barani Afrika kama miongoni mwa mikakati ya kukuza kasi ya maendeleo na demokrasia. “Kupitia mafunzo, mijadala na kubadilishana uzoefu, vyombo vya habari vitaweza kusaidia nchi za ...