Wasaidieni wananchi kufikisha malalamiko uvunjifu haki za binadamu - Awami


RAHMA KHAMIS NA ISSA MZEE, MAELEZO

Waandishi wa habari Nchini wametakiwa kutoa habari zinazohusu uvunjifu wa haki za binaadamu ili kuwasaidia wananchi kufikisha malalamiko yao sehemu husika ili kukuza ustawi wa jamii nchini. 

Akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari katika warsha iliyoandaliwa na Mkufunzi kutoka  Shirika la Waandishi wa Habari wa  Haki za Binaadamu, Sami Awami, (aliesimama) katika Hoteli ya Golden Tulip, Kibweni alisema ipo haja kwa waandishi wa habari kupata mafunzo hayo ili kusaidia upatikananji wa haki za binadamu nchini.

Akiwasilisha mada ya haki za bindamu na ugonja wa corona amesema kuibuka kwa maradhi hayo duniani, kumesababisha kutokea kwa vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu kwa baadhi ya raia wa mataifa jambo ambalo limeleta athari kubwa kwa watu wengi hasa wananwake na watoto.

Akitoa mfano wa vitendo hivyo, vimejitokeza baada ya kuwekwa karantini iliyowekwa kwa baadhi ya mataifa amesema ubakaji kwa wanawake na watoto,kupigwa pamoja na unyang’anyi ni miongoni mwa vitendo vinavyofanyika nchi nyingi duniani.

Amesema kuwa  kutokana na muanguko wa kiuchumi uliosababishwa na corona umepelekea kutokea kwa vitendo hivyo na kuwataka waandishi wa habari kuzipa kipaombele  habari zinazohusu haki za binadamu ili kutomeza janga hilo Duniani.

Aidha amefahamisha kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoathirika na janga hilo na kupelekea kuzorota kwa uchumi wa mtu mmoja mmoja na kusababisha baadhi ya wanawake na watoto kuvunjiwa haki zao za msingi na kudhalilishwa.

Alifafanua kuwa kutokana na kutojua haki na sheria ya haki za binadamu ya Tanzania na uwepo wa baadhi ya viongozi wanaokiuka sheria ni miongoni mwa sababu zinazopelekea vitendo vya uvunjivu wa haki za binadamu ikiwemo udhalilishaji.

Amefahamisha kuwa ni wajibu wa kila mtu duniani kote kupata haki za msingi za  binaadamu na kuwataka wandishi wa habari kuisaidia jamii katika kufahamu haki zao za  msingi ili kuondokana na vitendo vya uvunjifu wa haki hizo.

Nao washiriki katika mafunzo hayo wameeleza kuwa wanawake ndio waathirika wakubwa wa vitendo vya uvunjifu wa haki za binaadamu kwani hufanyiwa vitendo mbali mbali ikiwemo kubakwa hivyo lazima waripoti habari hizo kusaidia kuviondoa.

Wamefahamisha kuwa katika kipindi cha mwanzo cha maradhi ya Corona jamii ilikuwa na hofu dhidi ya ugonjwan huo kutokana na ugeni wa maradhi hayo pamoja na athari zake na kupeleka watuhumiwa wengi wa maradhi hayo  kunyanyapaliwa jambo ambalo ni uvunjivu wa haki za binadamu.

Wakizungumzia kuhusu haki za mwananchi, washiriki hao wamesema kuwa jamii bado haijui haki na wajibu wa kujikinga na kujilinda kutokana na maradhi hayo hivyo ipo haja kwa Serikali kutoa elimu khusu haki za binadamu.

Aidha wamefahamisha kuwa katika kupambana janga hilo hakuna kubudi kwa vyombo vya habari na jamii kwa ujumla kutoa elimu zaidi na kuandaa vipindi vinavyohusu haki za binadamu na corona ili wananchi wapate haki zao licha ya kukumbwa na janga la hilo.

PICHA NA MAELEZO:

 

Mwandishi wa Habari wa Zbc Redio Hinja Haji Pongwa (wa pili kulia) akitoa mchango wake katika Mafunzo kuhusiana na Haki za Binaadamu na ugonjwa wa Covid 19 yaliofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip, Kibweni jijini Zanzibar. (PICHA NA YUSSUF SIMAI, MAELEZO ZANZIBAR).

Comments

Popular posts from this blog

ZALIRI, FLI zaingia makubaliano kuimariusha sekta mifugo

Ibueni changamoto zinazokamisha usawa wa kijinsia - Simbaya

Uislam unakubali uzazi wa mpango