UZINDUZI WA MPANGO WA UWEZESHAJI MADEREVA BODABODA, BAJAJI ULIOFANYIKA KATIKA HOTELI YA UBUNGO PLAZA DAR ES SALAM

Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi, Biashara ndogo na za Kati Benki ya NMB,  Filbert Mponzi, akitoa maelezo juu ya mpango wa uwezeshaji madereva bodaboda na bajaji wakati wa uzinduzi wa mpango huo hafla hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Ubungo Plaza, Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akifurahia jambo pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB,  Ruth Zaipuna (kushoto). Kulia ni Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi, Biashara ndogo na za Kati Benki ya Nmb, Filbert Mponzi.


Waziri Jenista Mhagama (katikati) akizungusha bango kuashiria uzinduzi wa mpango wa uwezeshaji wa mikopo kwa madereva Bajaji na Bodaboda ijulikanayo kwa 'NMB MASTABODA – MILIKI CHOMBO'. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB,  Ruth Zaipuna (wa pili kutoka kulia). Kushoto ni Mwenyekiti wa Madereva Bodoboda,  Michael Massawe na Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi, Biashara ndogo na za Kati Benki ya Nmb, Filbert Mponzi.

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akionesha funguo za bodboda kabla ya kumkabidhi mmoja ya madereva wakati wa hafla ya Uzinduzi wa mpango wa uwezeshaji wa fursa za mikopo kwa madereva Bajaji na Bodaboda ujulikanayo kama 'NMB MASTABODA – MILIKI CHOMBO, iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo Ubungo Plaza, Jijini Dar Es Salaam.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu),  Jenista Mhagama akiwa amepakiwa kwenye pikipiki na mwendesha Bodaboda mara baada ya kuzindua rasmi fursa ya mikopo kwa madereva Bodaboda na Bajaji kupitia NMB MASTABODA – MILIKI CHOMBO.



☝Baadhi ya watendaji wa benki ya NMB, Madereva Bajaji na Bodaboda walioshiriki katika hafla hiyo wakisikiliza kwa makini hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama.👇


PICHA KWA HISANI YA OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, URATIBU, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU.



Comments

Popular posts from this blog

ZALIRI, FLI zaingia makubaliano kuimariusha sekta mifugo

Ibueni changamoto zinazokamisha usawa wa kijinsia - Simbaya

Uislam unakubali uzazi wa mpango