Waandishi watakiwa kuelimisha jamii chanjo ya kipindupindu

NA KHADIJA KHAMIS, MAELEZO

 

WAANDISHI wa Habari Zanzibar wametakiwa kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na chanjo ya Kipindupindu ili kujenga uelewa juu ya umuhimu wa chanjo hiyo.

 

Akifungua mafunzo kwa  waandishi wa habari kuhusu chanjo hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Zanzibar, Dkt. Abdallah Ali Suleiman (pichani), amesema  lengo la mafunzo hayo ni kutoa elimu kwa jamii ili kuondokana na  dhana potofu zinazotokana na chanjo hiyo

 

Amesema chanjo hiyo haina madhara kwa binadamu na inatolewa kwa ajili ya kuikinga jamii na maradhi ya mripuko hivyo ameitaka kuondoa shaka hiyo.

 

Ameeleza kuwa chanjo hiyo inatarajiwa kutolewa kwa mwezi ujao katika shehia mbali mbali za Unguja na Pemba kwa maeneo ambayo huathirika sana kila unapotokea mripuko wa maradhi hayo.

 

Nae Afisa Afya ya Jamii, Fauza Mohamed Abdulkadir, amesema chanjo hiyo inatarajiwa kutolewa kwa watu wenye umri wa mwaka mmoja na kuendelea na wagonjwa wenye maradhi sugu yasiyoambukizwa yakiwemo presha sukari na mengineyo.

“Chanjo hiyo haitopaswa kupewa wagonjwa mahatuti na mama wajawazito na watoto chini ya mwaka mmoja,” alifahamisha Afisa huyo.

 

Kwa upande wake Mratibu wa chanjo kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Vendelin Simon, amesema kuwa chanjo iko salama tayari imeshatolewa katika nchi mbalimbali  na haijaleta madhara yoyote kwa waliotumia ambayo ni dawa ya  kunywa sio sindano hivyo ameisihi jamii kuwa na mwamko wa kushiriki kupata chanjo hiyo.

 

Zoezi la utoaji wa chanjo ya kipindupindu linatarajiwa kufikia zaidi ya watu 300,000 katika Wilaya tisa za Unguja na Pembazenye jumla ya shehia 58 ikiwa na lengo la kutoa kinga kwa wananchi katika kipindi cha  miaka mitatu hadi mitano.


PICHA


Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Jamii wa Wizara ya Afya Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Zanzibar, Dkt. Fadhil Mohammed Abdalla akaimkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa Wizara hiyo kufungua mafunzo ya siku moja kwa Waandishi wa Habari wa habari kuhusu chanjo ya kipindupindu yaliyofanyika Ukumbi wa ZSSF Kariakoo Mjini Zanzibar.



Mratibu wa Chanjo ya Kipindupindu Zanzibar Dkt.Vendelin Simon kutoka shirika la afya duniani (WHO) akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari (hawamo pichani) kuhusu chanjo ya kipindupindu katika mafunzo ya waandishi wa habari yaliyofanyika katika ukumbi wa ZSSF Kariakoo, Zanzibar. (PICHA NA FAUZIA MUSSA, MAELEZO – ZANZIBAR).


Waandishi wa habari wa Vyombo mbalimbali wakifuatilia mafunzo kuhusu chanjo ya kipindupindu yaliyotolewa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) kupitia kitengo cha maradhi yasiyoambukiza yaliyofanyika katika ukumbi wa ZSSF Kariakoo, Zanzibar.


WADAU wa Afya, Viongozi na Watendaji wa Wizara ya Afya wakiwa katika picha ya pamoja na Waandishi wa Habari wa Vyombo mbali mbali baada ya mafunzo ya siku moja kuhusu kampeni ya chanjo ya kipindupindu yaliyofanyika katika ukumbi wa ZSSF, Kariakoo Zanzibar.(PICHA NA FAUZIA MUSSA, MAELEZO – ZANZIBAR).

Comments

Popular posts from this blog

ZALIRI, FLI zaingia makubaliano kuimariusha sekta mifugo

Ibueni changamoto zinazokamisha usawa wa kijinsia - Simbaya

Uislam unakubali uzazi wa mpango