Wanachama Yanga SC wakubali mabadiliko

NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAM

WANACHAMA wa Klabu ya Yanga ya jijini Dar es salam wamekubali rasmi kuingia katika mfumo wa mabadiliko ya uendeshaji na mabadiliko ya katiba kwenye mkutano mkuu uliofanyika Juni 27, mwaka huu.

Mwenyekiti wa Yanga, Dk. Mshindo Msolla akiongoza mkutano huo, aliwauliza wanachama kuhusu kuafiki mabadiliko hayo mara baada ya kutambulisha kamati iliyosimamia mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji.

Wajumbe 1,170 ambao walijiandikisha katika Mkutano Mkuu uliofanyika katika ukumbi wa DYCC, jijini Dar es Salaam walipitisha mabailiko hayo kwa kura za ndio.

Baada ya Dk. Msolla kuwauliza wanachama wanaoafiki mabadiliko hayo na ukumbi mzima ukanyoosha mikono akiwamo, Rais mstaafu wa awamu ya nne, Dk. Jakaya Kikwete, aliyekuwa mgeni rasmi huku baadhi yao wakipiga kelele kuwa wote wanaafiki.

Baada ya hatua hiyo, Dk. Msolla aliwakabidhi vyeti wajumbe wa kamati hiyo na kisha akarejea tena kwa wanachama kuwauliza wasioafaki na hakuna mkono ulionyooshwa.

Sehemu ya mabadiliko kwa klabu ya Yanga ni kuifanya timu hiyo kuwa kampuni huku klabu ikimiliki hisa aslimia 51 na wawekezaji wakimiliki hisa asilimia 49.

Comments

Popular posts from this blog

ZALIRI, FLI zaingia makubaliano kuimariusha sekta mifugo

Ibueni changamoto zinazokamisha usawa wa kijinsia - Simbaya

Uislam unakubali uzazi wa mpango