
GeSCI kuzindua mpango kuimarisha elimu Tanzania NA MWANDISHI MAALUM MPANGO kutathmini utungaji na utekelezaji wa sera za elimu nchini Tanzania unatarajiwa kuzinduliwa Machi 24, 2022 katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort Zanzibar. Taarifa iliyotolewa na taasisi ya Global e-Schools and Communities Initiative (GeSCI), ameeleza kuwa mpango huo unaotekelezwa na chuo kikuu cha Makerere, Uganda na Kituo cha Kimataifa cha Chuo Kikuu cha Notre Dame, umelenga kufanya tafiti, tathmini na kutafsiri sera za ufundishaji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Taarifa hiyo imeeleza kuwa kupitia mpango wa Tathmini ya Kurekebisha sera za kufundishia (ADAPT), utafiti unafanyika ili kufikia malengo ya kutoa mafunzo kitaifa na kikanda ili kuimarisha maamuzi ya kitaifa yanayotokana na takwimu. Katika uzinduzi huo, miongoni mwa wageni watakaohudhuria na kuwasilisha taarifa na mada ni pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Tanzania Bara Prof. Eliamini Sedoyeka, Katibu Mkuu Wizara ya...