Programu kuratibu maudhui ya filamu kuanzishwa

NA SAIDA ISSA, DODOMA

Na Saida Issa, Dodoma 

SERIKALI kupitia kamati ya kutetea haki za wasanii inatarajia kuanzisha programu ya kuratibu uandaaji wa filamu zenye maudhui ya kutangaza utajiri wa nchi katika eneo la utamaduni, historia na jiografia yake.

Hayo yalibainishwa jijini hapa jana, na Katibu Mtendaji wa  Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) Dk. Kiagho Kilonzo (pichani) wakati akizungumza na wandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa shughuli za bodi na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti ya mwaka huu wa fedha.

Amesema hadi sasa Kamati ya kutetea Haki za Wasanii imeshapokea malalamiko 30 na kuyashughulikia, huku takribani sh. milioni 300 zilizokuwa zimedhulumiwa zimesharejeshwa kwa wasanii.

Alisema lengo la filamu hiyo ni  kujenga mapenzi hasa kwa vijana wa kitanzania kwa nchi yao kwa kuwaongezea ufahamu wa rasilimali waliyonayo.

“Programu hii itasaidia kutunza kumbukumbu za kihistoria kwa kuhusisha taarifa za viongozi wetu mbalimbali waliofanya mambo makubwa kama vile Mwl. Julius  Nyerere ambaye alisaidia ukombozi wa nchi mbalimbali barani Afrika,”alisema.

Kuhusu haki na maslahi ya wasanii Dk. Kilonzo alisema TFB  inaratibu kamati maalum ya kutetea haki za wasanii iliyoundwa na Waziri mwenye dhamana ya kusimamia maswala ya sanaa nchini kwa mara ya kwanza mwaka 2018 na kuhuishwa tena 2019 na 2020 itakayodumu hadi mwishoni mwa mwaka 2022.

Alisema hadi sasa Kamati imeshapokea malalamiko 30 na kuyashughulikia, ambapo takriban sh. milioni 300 zilizokuwa zimedhulumiwa zimesharejeshwa kwa wasanii.

“Malalamiko 22 yamesuluhishwa, na malalamiko nane yapo katika hatua mbalimbali za kushughulikiwa  baadhi ya malalamiko yaliyopokelewa na kushughulikiwa ni yale ya marehemu Amri Athumani (King Majuto), marehemu Steven Kanumba, msani David Ganzi (Young Dee), Mzalishaji wa Tamthilya Samwel Isike ambayo yalitokana na kuingia mikataba mibovu.,”alifafanua.

Katika hatua nyingine Dk.Kilonzo alisema TFB imeendelea kuongeza wigo wa utoaji ajira ambapo kwa kipindi cha Januari hadi Disemba mwaka jana  inakadiriwa kuwa ilichangia takriban ajira 30,000 zilizotokana na Filamu.

Alisema kwa mazingira ya Kitanzania, Filamu moja inakuwa na wastani wa watu 20, tamthiliya moja wastani wa watu 100.

“Kiasi hicho ni ongezeko la nafasi 5,000 kutoka 25,000 kiasi kinachokadiriwa kuzalishwa mwaka 2020 hadi kufikia ajira 30000 ambazo zimezalishwa mwaka jana na kwa mwaka huu tunatarajia takwimu hizo kuongezeka kwa wingi kwasababu tasnia imekuwa,”alieleza

Comments

Popular posts from this blog

ZALIRI, FLI zaingia makubaliano kuimariusha sekta mifugo

Ibueni changamoto zinazokamisha usawa wa kijinsia - Simbaya

Uislam unakubali uzazi wa mpango