Wanafunzi MCC, MSJ watakiwa kusoma kwa bidii

NA ASYA HASSAN WANAFUNZI wanaosomea fani ya habari katika chuo cha Mwenge Community Center (MCC) na Morogoro School of Journalis (MSJ) wametakiwa kusoma kwa bidii ili kuwa wataalamu wazuri wa fani ya habari wanapomaliza masomo yao. Mwenyekiti wa KLABU ya Waandishi ya Habari Zanzibar (ZPC), Abdallah Abdulrahman Mfaume, alitoa rai hiyo alipokuwa akizungumza na wafunzi hao chuoni kwao Amani, ikiwani mwendelezo wa shughuli za maadhimisho ya miaka 30 Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani iliyoadhimishwa Mei 3, mwaka huu. Alisema hatua hiyo itawasaidia kuwa ujasiri katika kutekeleza vyema majukumu ya kuisemea jamii kwaniu tasnia hiyo ni muhimu katika kuchochea maendeleo na ustawi wa jamii. “Leo mpo chuoni lakini mtakapotoka hapa mtakwenda kuitumikia jamii hivyo kuna umuhimu kwenu kujikita katika masomo ili maarfa mnayoyapa mkayatumie kuimarisha ustawi wa jamii na maendeleo ya nchi”, alieleza Mfaume. Sambamba na hayo aliwataka waandishi wa habari hapa nchini kuacha mihemko wanapo...