Dk. Mwinyi aipongeza Amref misaada sekta ya afya

NA MWANDISHI WETU

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amelipongeza shirika la AMREF Afrika Tanzania kwa kuendeleas kutoa msaada kwa serikali kuimarisha afya ya mama na mtoto kupitia programu ya Uzazi ni Maisha Wogging.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, mama Mariam Mwinyi, Naibu Waziri wa Afya, Khamis Hafidh na Mkurugenzi Mtendaji wa Amref Afrika Tanzania, Dk. Florence Temu

Dk. Mwinyi alitoa pongezi hizo mara baada ya kushiriki matembezi ya hiyari na mbio fupi yenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kununulia vifaa tiba vitakavyotumika katika hospitali na vituo vya afya vya maeneo mbali mbali ya Zanzibar ili kupunguza vifo vya Mama na Mtoto Zanzibar


Dk. Mwinyi ameeleza kuwa jitihada zinazochukuliwa na wadau wa maendeleo, wahisani na mashirika ya ndani nay a kimataifa yanaongeza uwezo wa serikali katika kuhudumia watu wake hivyo zinapaswa kupongezwa na kuungwa mkono.

Alisema licha ya serikali kujenga miundombinu ya kutolea huduma za afya bado sekta ya afya inakabiliwa na changamoto ya uchache wa vifaa hivyo kampeni hiyo ya miaka mitatu ina mchango mkubwa kwa maendeleo ya sekta hiyo na uimarishaji wa afya za wamama wajawazito na watoto.


Mkurugenzi Mkaazi wa Amref Afrika Tanzania Dk. Florence Temu,akimvisha medali rais wa zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi baada ya kushiriki matembezi ya Uzazi ni Maisha Wogging Marathon  

Dk. Mwinyi alisema ' Uzazi ni Maisha Wogging Marathon (Walk-Jog-Run) kwa mwaka 2023’ iliyoandaliwa kwa ushirikiano baina ya wizara ya Afya Zanzibar na Shirika la Kimataifa la Amref Health Afrika Tanzania chini ya ufadhili wa benki ya ABSA na wadau wengine ni tukio linalotoa nafasi ya kila mmoja miongoni mwa jamii kutoa mchango wake hivyo aliwasihi wananchi na wadau kuendelea kuiunga mkono serikali ili kukabiliana na changamoto mbali mbali.

Dk. Mwinyi akihutubia washiriki wa Uzazi ni Maisha Wogging Marathon 

“Wadau wa maendeleo na mashirika yana mchango mkubwa katika kusaidia maendeleo ya jamii hivyo nalipongeza shirika la Amref Tanzania  kwa kuanzisha kampeni ya 'Uzazi ni Maisha Wogging yenye lengo la kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga”, alieleza Dk, Mwinyi.

Aidha alilipongeza Amref Health Africa kwa kutoa msaada wa gari maalum ambayo itasaidia kusafirisha wataalamu, kusafirisha sampuli, kutoa huduma za upimaji na ushauri nasaha kwa wananchi katika vituo vya afya vya Zanzibar.

Aliongeza kuwa takwimu za mwaka 2017, zinaonesha vifo vya kina mama 134 kati ya vizazi hai 100,000 kwa mwaka na vifo 28 vya watoto wachanga kati ya vizazi hai 1,000, ambapo husababishwa na changamoto za huduma duni za mama na mtoto katika hospitali na vituo vya afya zikiwemo uhaba wa wahudumu a tatizo la kukosekana kwa dawa.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi (wa pili kulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kliniki inayotembea kwa ajili ya kutoa huduma za mama na mtoto. Kulia ni Mke wa Rais mama Mariam Mwinyi.

Dk. Mwinyi, alieleza matumaini yake kupitia kampeni hiyo, kwamba serikali itaongeza vifaa tiba kwa vituo vya afya 28, sawa na asilimia 40.5 ya vituo vote 69 vinavyotoa huduma za mama na mtoto Zanzibar.

Akizungumza kwenye hafla hivo, Naibu Waziri wa Afya, Hassan Khamis Hafidh, alisema lengo la kuanzishwa kwa kampeni ya "Uzazi ni Maisha" ni kupunguza vifo vya mama wajawazito a watoto chini.

Alisema, katika kulikabili tatizo hilo kivitendo, serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeweka mikakati ikiwemo kuwachukulia hatua kali za kisheria na nidhamu watumishi wote wa sekta ya afya wanaokiuka sheria na taratibu za utumishi kutokana na uzembe kazini.

Dk. Mwinyi akipokea tunzo ya kutambua mchango wake katika kuimarisha sekta ya afya tioka kwa Mkurugenzi Mkaazi wa Amref Afrika - Tanzania, D. Florence Temu.

Aidha alisema serikali haitovumilia kauli chafu kutoka kwa watendaji wa sekta ya afya, utovu wa nidhamu unaosababisha athari maya kwa mama na watoto hasa wakati wa kujifungua.

Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini Tanzania, Zlatan Milisic alisema “Tunashukuru kwa kupata fursa ya kuwa sehemu ya hafla hii iliyoandaliwa na Amref na Wizara ya Afya Zanzibar, michango itokanayo na mpango huu wa Uzazi Ni Maisha Wogging  wa kuchangisha fedha yatakwenda katika ununuzi wa vifaa tiba ili kuboresha huduma za afya na kuokoa maisha ya mama na mtoto Zanzibar”.

Aliongeza kuwa; “Wakati maendeleo yamepatikana, bado kuna kazi kubwa ya kupunguza viwango vya vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga.Umoja wa Mataifa bado una nia ya dhati ya kusaidia Tanzania na Zanzibar katika jambo hili muhimu.Kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko na kutoa huduma bora za afya na matunzo kwa akina mama na watoto wachanga”.

Naye, Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la Amref Health Afrika kwa upande wa Tanzania, Dk. Florence Temu, alisema lengo la kuanzishwa kampeni hiyo ni kukusanya shilingi bilioni moja kwa ajili ya kununulia vifaa tiba vya hospitali na vituo vya afya 69 vinavyotoa huduma za mama na mtoto, Zanzibar.


Alisema, wakiwa mwenye mwaka wa pili wa kampeni yao, Shirika la Amref Health Afrika tayari limefanikiwa kukusanya shilingi milioni 557 na wamepokea ahadi za shilingi milioni 883 ambayo itafikisha lengo la kampeni hiyo kufikia 2024.

Kampeni ya "Uzazi ni Maisha" ilianza mwaka jana na inatarajiwa kukamilika mwakani inatekelezwa kwa kaulimbiu isemayo" changia vifaa tiba kwa uzazi salama" ambayo imechangia kufikia malengo ya kuanzishwa kwake mwaka wa pili sasa wa utekelezaji wake

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Absa, Obedi Laiser alisema ushirika kati ya Amref na ABSA ulikuwa na thamani kubwa na kiasi kilichochangwa na benki ni mwendelezo wa juhudi za benki hiyo katika kutimiza sera yake ya kurudisha kiasi cha faida Kwa jamii (CSR) kunakosukumwa na utayari wa kushirikiana na jamii ambako benki inatoa huduma ili kuimarisha sekta ya afya.


Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya ABSA, Obedi Laiser, akitoa salamu za benki hiyo ambayo ni mdhamini mkuu wa mbio na matembezi hayo.

Comments

Popular posts from this blog

ZALIRI, FLI zaingia makubaliano kuimariusha sekta mifugo

Ibueni changamoto zinazokamisha usawa wa kijinsia - Simbaya

Uislam unakubali uzazi wa mpango