ZBS yachangia kambi ya matibabu ya ZMBF

NA MWANDISHI WETU TAASISI ya Viwango Zanzibar (ZBS) imeeleza kuwa itaendelea kushirikiana na wadau mbali mbali ili kuimarisha ustawi wa jamii na uchumi kupitia njia mbali mbali. Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo, Yusuph Majid Nassor, alieleza hayo jana wakati akikabidhi msaada wa vifaa vya uchunguzi na matibabu kwa taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) kwa ajili ya kambi ya uchunguzi wa afya na matibabua itakayofanyika kuanzia Septemba 30 hadi Oktoba 2, mwaka huu. Yusuph alieleza kuwa hatua hiyo inaangukia katika moja ya maeneo yanayosaidiwa na taasisi yake kupitia mpango wa kusaidia jamii na wadau wake ikiwemo taasisi hiyo ambayo ni miongoni mwa wateja wake. “Kila mwaka huwa tunatoa sehemu ya mapato tunayokusanya kwa jamii na tumelkua tukipeleka msaada kwa wizara ya afya na kwa mwaka huu tunaelekeza sehemu ya mapato hayo katika tukio hili kuiunga mkono ZMBF lakini pia wizara ya afya”, alieleza Yussuph. Hata hivyo aliahidi kuwa taasisi yake itaendelea kusaidia shughuli ...