Dk. Samia ainua hali za wakulima wa korosho Lindi

NA MWANDISHI WETU IMEELEZWA kuwa hatua ya Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kupandisha bei ya korosho ni miongoni mwa ahadi alizozitoa kuimarisha maisha ya wakulima kwa kuwapatia bei nzuri ya mazao yao. Akizungumza wakati wa mnada wa 10 wa zao hilo, Ofisa usimamizi wa fedha wa Soko la Bidhaa Tanzania(TMX), Prince Mng'ong'o, alieleza kuwa hali hiyo inakwenda sambamba na kuongeza ununuzi wa zao hilo lililofikia tani 401,000 zenye thamani ya shilingi Trilioni 1.44 kwa mwaka 2024/2025. Alieleza kuwa mafanikio hayo ni pamoja na kupandishwa kwa bei ya zao hilo, yameongeza thamani kwa mkulima na kupandisha uchumi wa Taifa ambapo wakati msimu wa ununuzi wa korosho kwa mwaka 2024/2025 ukikaribia kumalizika mpaka sasa kiasi hicho cha tani hizo za Korosho zimenunuliwa. Katika Mnada wa kumi wa chama Kikuu cha Ushirika cha RUNALI kwa msimu wa 2024/2025 uliofanyika Mjini Nachingwea, Mng'ong'o alisema, hadi sasa kiasi hicho cha tani za korosho...