Mama Samia amwaga mamilioni ujenzi kampasi ya TIA Z’bar
NA MWANDISHI WETU
SERIKALI y Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Dk. Samia Suluhu Hassan, imetoa kiasi cha shilingi bilioni 30 kwa ajili ya ujenzi wa ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), kmpasi ya Zanzibar.
MSIMAMIZI wa ujenzi wa mradi wa Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA), kutoka kampuni ya Salem Constructions, Muhandisi Riziki Ringo (katikati) akitoa maelezo kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo, Profesa Willian Amos Pallangyo, alipotembelea kukagua ujenzi wa mradi huo unaoendelea shehia ya Nganani, Makunduzi Kusini Unguja.
Awamu ya kwanza ya ujenzi huo umeanza toka mwezi Septemba mwaka huu ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono dhamira ya serikali zote mbili za Tanzania kuhakikisha wananchi wa pande zote mbili za muungano wanafaidika na taaluma bora inayotolewa vyuo ya taasisi za elimu zilizopo nchini.
Afisa Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo, Profesa Willian Amos
Pallangyo, alieleza hayo baada ya kukagua awamu ya kwanza ya ujenzi wa
kampasi hiyo inayojengwa shehia ya Ng'anani Makunduchi, mkoa wa akusini Unguja.
Amesema ili kukamilisha ujenzi huo Serikali ya Jamuhuri ya
Muungano imetoa kiasi hicho cha fedha huku erikali ya Mapinduzi Zanzibar ikitoa eneo lenye ukubwa wa hekta
56 hivyo watahakikisha wanalitendea haki
eneo hilo kwa kutumia vyema fedha zilizotolewa na kukamilisha ujenzi huo kwa
muda uliopangwa.
Profesa Pallangyo amesema kukamilika kwa ujenzi huo wanategemea
kuwa na wanafunzi wasiopungua 1,500 watapata huduma mbali mbali zikiwemo za kumbi
za mihadhara, vyumba vya maktaba na komputa na
mabweni ya wanafunzi wa kike na kiume zaidi ya 480.
“Nimeridhika kwa hatua zilizofikiwa katika awamu ya kwanza na
niahidi kulitendea haki eneo hili kwa kuhakikisha tunatunza mazingira yake na
kulifanyia kazi kama ilivyokusudiwa kwani serikali imetambua sekta ya elimu na
kwa sasa imekuwa ikikua zaidi”, alieleza Prof. Pallanyo.
Kwa upande wake, Naibu Mkuu wa chuo hicho, Mipango, Fedha na
Utawala, Dk. Issaya Hassanal, alisema ujenzi huo unatarajiwa kukamilika mwaka
2026 na kutoa faida za kiuchumi kwa kupokea wanafunzi kutoka Tanzania bara,
Zanzibar na mataifa ya kigeni ambayo wataitumia taasisi kwa ajili ya kupata
elimu.
Aidha alisema ujenzi huo pia utawasaidia wananchi wa eneo
hilo kupata ajira za muda na za kudumu zikiwemo za ufundi na vibarua wa ujenzi
pamoja na mamantilie kupata kuuza biashara zao.
Naye, Msimamizi wa ujenzi wa mradi huo kutoka kampuni ya Salem
Constructions, Muhandisi Riziki Ringo, alisema mradi huo wa miaka miwili walikabidhiwa
mwezi Septemba, mwaka huu unaendelea vyema na kuahidi kuwa watatekeleza kwa
wakati licha ya kuwepo kwa changamoto ndogo ndogo.
Ujenzi huo unatarajiwa kujengwa kwa awamu mbili ambapo awamu
ya kwanza unaoendelea hivi sasa unaohusisha mabweni ya wanafunzi na madarasa
pamoja na ofisi, utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 13.5
Comments
Post a Comment