JUWAZA kuhamasisha upatikanaji haki za wazee

NA MWANDISHI WETU JUMUIYA ya Wastasfu na Wazee Zanzibar (JUWAZA) imesema itaendelea kuhamasisha upatikanaji wa stahiki za wazee zikiwemo za kiafya ili kupata haki zao na afya zao zinaimarika. Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari ofisini kwake Migombani, Katibu wa jumuiya hiyo, Salama Kondo Ahmed, alisema jumuiya imekuwa ikitekeleza kazi zake kwa mashirikiano na serikali pamoja na taasisi binafsi katika kuhakikisha inafikia malengo yake. Alisema kuwa idadi ya watu wenye umri wa miaka 80 na kuendela inakadiriwa kukua kwa mara tatu zaidi baina ya mwaka 2022 na 2050 na kufikia milioni 426 ulimwenguni hivyo nchi zinahitaji kujiandaa na kuandaa mazingira ya kukidhi mahitaji ya wazee. Kondo alisema, JUWAZA ina mikakati mbali mbali ya kuimarisha ustawi wa wazee na wastaafu itakayotekelezwa kwa ushirikiano na serikali na taasisi binafsi “Miongoni mwa mambo ambayo tumeweza kuyasimamia ni pamoja na kufanya utetezi na kupelekea kuuanzishwa kwa mpango wa pensheni jamii kwa wazee wo...