Wadau TIB watakiwa kuimarisha mashirikiano

NA MWANDISHI WETU WADAU wa Benki ya Maendeleo nchini (TIB) wametakiwa kuimarisha mashirikiano ili kuongeza mchango wa benki hiyo katika maendeleo ya taifa. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila (kushoto) akisalimiana na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Maendeleo TIB, Agapiti Kobello (wapili kushoto) wakati alipowasili kufungua Mkutano wa Wadau wa Benki ya Maendeleo (TIB) Kanda ya Dar es Salaam uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam. Wengine ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TIB, Juma Hassan Reli (watatu kushoto), Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIB, Lilian Mbassy (wapili kulia) na Kaimu Mkurugenzi wa Usimamizi wa Miradi, Zuwena Hemed (kulia). Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila wakati akifungua mkutano wa majadiliano uliowakutanisha watendaji na wadau wa benki hiyo wa kanda ya Dar es salaam ulioangalia majukumu na mafanikio ya benki hiyo katika kuchangia maendeleo nchini...