Maafisa Habari Z'bar watakiwa kuongeza kasi ya uwajibikaji

NA MWANDISHI WETU WAZIRI wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo, Tabia Maulid Mwita, amewataka Maofisa Habari na Mawasiliano wa wizara na taasisi za serikali kutekeleza majukumu yao vyema na kutoa taarifa za utendaji wa serikali kwa wananchi. Waziri Tabia alieeleza hayo jana katika ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil, Kikwajuni, mjini Unguja wakati wa uzinduzi wa Jumuiya ya Maafisa Habari na Mawasiliano Zanzibar (ZICCO) na kusema maafisa hao na watu binafsi wana jukumu la kuhakikisha kuwa wananchi wanapata habari za taasisi zao kwa wakati na usahihi. "Kuna miradi mingi ya maendeleo inafanyika katika taasisi zenu lakini wananchi hawaelewi kutokana na taasisi hizo kukaa kimya bila kuijulisha jamii", alisema Waziri Tabia. Alifafanua kuwa kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, kifungu 18 (1 na 2) kinatoa uhuru kwa kila mtu kuwa na haki ya kupokea na kutoa habari na kinaonesha haki ya raia kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio yanayofanyika nchini na duni...