ZAMECO yakumbushia sheria mpya ya habari
NA MWANDISHI MAALUM KAMATI ya Wataalamu y a Vyombo vya Habari Zanzibar (ZAMECO), ime i shauri serikali kukamilisha mchakato wa upatikanaji wa sheria mpya ya habari ili kuimarisha uhuru wa kujieleza na uwajibikaji . Akizungumza wa kati w a kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani upande wa Zanzibar, lililofanyika Rahaleo Studio , Mjumbe wa ZAMECO, Salim Said Salim, alisema mchakato huo umechukua muda mrefu hivyo ipo haja ya kuchukuliwa kwa hatua za makusudi kuukamilisha. “Katika miaka ya hivi karibuni tu me shuhudia sheria nyingi zikipitishwa na Baraza la Wawakilishi ila sheria ya habari mchakato wake umekuwa ukienda na kurudi kwa zaidi ya miaka 20 hali inayowafanya wadau wa tasnia ya habari ku jion a wanyonge ”, alisema Salim. BAADHI ya waandishi wa habari na wafdau wa habari wakifuatilia uwaasilishaji wa mada wakati wa kongamano Aliziomba mamlaka zinazohusika kuendelea kushirikiana na taasisi za kihabari kuhakiki...