Posts

Wanahabari wanawake wapewa mbinu kukwepa udhalilishaji mitandaoni

Image
NA AMINA MCHEZO WAANDISHI wa habari wanawake wananafasi na mchango mkubwa katika kuielimisha jamii kupitia mitandao ya kijamii kukizingatiwa usalama wao . Akifungua mafunzo ya siku mbili  kwa waandishi wa habari wanawake Zanzibar, Mkufunzi na mwanahabari mkongwe kutoka nchini Kenya,  Cecilian Maundu (pichani), amesema wanahabari wanawake wamekuwa wakipitia wakati mgumu wakiwasilisha kazi zao za kimtandao ukilinganisha na wanahabari wa kiume. Amesema hali hiyo huwawia vigumu baadhi ya waandishi kuendelea na kazi yao na wengine kuathirika kisaikolojia kutokana na baadhi ya wafuasi wa kimtandao kuwatolea maneno ya kashfa pasi na wao kuridhia. Maundu amesema hali hiyo inaweza ikaondoka au kusaidiwa endapo kutakuwa na ushirikiano wa pamoja kati ya waandishi na taasisi za kihabar ili kuunda kikosi kazi ambacho kitamlinda mwandishi pale tu anapopata kadhia ya kimtandao. "Zanzibar mnapaswa kutumia taasisi hizi kama ZPC, TAMWA, MCT na nyengine ili pale kuona mnashambulia Kwa ...

Zaipuna awapa msukumo vijana kuikabili changamoto za karne ya 21

Image
NA MWANDISHI WETU AFISA Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, amewashauri vijana nchini kunoa ujuzi wao wa karne ya 21 ili kufanikiwa katika soko la kisasa la ajira lenye ushindani. Akizungumza katika mahafali ya wanafunzi wa kidato cha nne wa skuli za sekondari za Feza yaliyofanyika jijini Dar es salam mwishoni mwa wiki, Zaipuna alisema ujuzi wa Karne ya 21 ni pamoja na kufikiri kwa kina, ubunifu, ushirikiano, mawasiliano, tekinolojia ya habari, uongozi, na stadi za maisha. “Mkiwa na ujuzi huu, nina hakika kabisa kwamba mtafaulu katika shughuli zenu za maisha iwe mnataka kuajiriwa au kujiajiri. Mtawavutia waajiri na wawekezaji na kwa moyo wa kuendelea kujifunza, mtaimarika siku hadi siku na kujiongezea thamani,” Zaipuna alisema. Aliongeza, “Kwa miaka mingi, nimekuwa sehemu ya Shule za Feza na ninathamini sana msisitizo ambao shule inaweka katika elimu ya maisha na maendeleo, ushirikiano na jamii na ukuzaji wa stadi za uongozi, sifa ambazo naamini zitakuwa na athiri chanya...

SERIKALI YA DK. SAMIA IMEKUZA USAWA WA KIJINSIA - MAJALIWA

Image
NA MWANDISHI MAALUM WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kazi kubwa imefanyika katika kipindi cha awamu hii ya uongozi kwa kutekeleza mikakati na sera zinazolenga kuondoa ubaguzi na kukuza usawa wa kijinsia.  Ametoa kauli hiyo Jumapili, Desemba 3, 2023 wakati akizungumza na maelfu ya wananchi waliohudhuria kilele cha maadhimisho ya tatu ya kumbukumbu ya kumuenzi mwanasiasa mkongwe, Bibi Titi Mohammed yaliyofanyika kwenye viwanja vya Ujamaa, Ikwiriri, wilayani Rufiji, mkoani Pwani.  Waziri Mkuu ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan alisema: “Pamoja na jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali, asasi za kiraia na jumuiya ya kimataifa, bado kuna changamoto nyingi katika kufikia usawa wa kijinsia. Ukweli huo unatoa msukumo muhimu wa kuendeleza na kuimarisha juhudi zetu katika kushughulikia masuala ya usawa wa kijinsia”, amesema. Akitaja baadhi ya hatua zilizochukuliwa na Serikali ya awamu ya sita, Waziri Mkuu amesema ya kwanza ni kuongeza idadi ya ...

Wadau TIB watakiwa kuimarisha mashirikiano

Image
NA MWANDISHI WETU  WADAU wa Benki ya Maendeleo nchini (TIB) wametakiwa kuimarisha mashirikiano ili kuongeza mchango wa benki hiyo katika maendeleo ya taifa. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila (kushoto) akisalimiana na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Maendeleo TIB, Agapiti Kobello (wapili kushoto) wakati alipowasili kufungua Mkutano wa Wadau wa Benki ya Maendeleo (TIB) Kanda ya Dar es Salaam uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam. Wengine ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TIB, Juma Hassan Reli (watatu kushoto), Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIB, Lilian Mbassy (wapili kulia) na Kaimu Mkurugenzi wa Usimamizi wa Miradi, Zuwena Hemed (kulia).   Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila wakati akifungua mkutano wa majadiliano uliowakutanisha watendaji na wadau wa benki hiyo wa kanda ya Dar es salaam ulioangalia majukumu na mafanikio ya benki hiyo katika kuchangia maendeleo nchini...

Vodacom yawapa uhakika wa matibabu mama, watoto wachanga

Image
NA MWANDISHI WETU KAMPUNI ya mawasiliano ya Vodacom imetoa zawadi ya bima kubwa ya afya kwa mama 100 na watoto wachanga 100 waliozaliwa na kulazwa katika hospitali ya rufaa ya Mnazimmoja, Zanzibar. Mama (mzazi)   Maryam Yohana Daniel (aliyeketi) akipokea bima kubwa ya afya kwa niaba ya wenzake wakati wa hafla ya ugawaji wa bima hizo kwa mama wazazi na watoto katika hospitali ya Mnazimmoja. Hatua hiyo ni sehamu ya kampeni ya kampuni hiyo ya kueneza upendo katika msimu wa sikukuu ambapo k ina mama waliojifungua kuanzia Novemba 9, mwaka huu katika hospitali hiyo watapatiwa bima ya ‘Voda Bima’. Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi bima hizo, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Annette Kanora (wa tatu kushoto), alisema hatua hiyo ni muendelezo wa mpango wa kampuni hiyo kuwashukuru wateja wake na kusaidia kupunguza changamoto zinazoikabili jamii.   Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Annette Kanora (wa tatu kushoto...

Enezeni elimu kupunguza uharibifu wa misitu – Shamata

Image
NA SALAMA MOHAMMED, WKUMM WAZIRI wa Kilimo Umwagiliaji Maliasili na Mifugo, Shamata Shaame Khamis, ameitaka Idara ya Misitu kuandaa mafunzo maalum kwa wanajamii, Taasisi za Serikali na Zisizo za kiserikali (NGO's) ili kupunguza uharibifu wa misitu. Ameeleza hayo shehia ya Bwejuu katika eneo la hifadhi ya Msitu wa Jamii Tongole, wilaya ya Kusini Unguja wakati alipokua akizindua zoezi la Upandaji wa miti asili kwenye msitu huo. Shamata amesema kuna baadhi ya watu wana mwamko mdogo wa kutunza misitu asili na hivyo kusababisha matatizo yakiwemo ya mabadiliko ya tabia nchi hivyo wakipatiwa elimu itawasaidia kuondokana na uharibifu huo.   Aidha amefahamisha kuwa lengo la hatua hiyo ni kudhibiti uharibifu wa msitu na uvamizi unaofanywa na watu kwa kufyeka miti kuandaa mashamba ya shughuli za kilimo, ujenzi na ujenzi wa makaazi usiozingatia taratibu na sheria za nchi.   "Nataka kuwakumbusha kwamba msitu huu umehifadhiwa na jamii chini ya sheria ya misitu namba 10 ya mwaka 1996...

Mama Mariam ahimiza lishe bora, mazoezi kujikinga na maradhi

Image
NA MWANDISHI MAALUM, LONDON MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) mama Mariam Mwinyi, amesisitiza umuhimu kwa jamii kubadili mtindo wa maisha kwa kuzingatia lishe bora, sambamba na kufanya mazoezi. MKE wa Rais wa Zanzibar, ambaye pia Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation, Mama Mariam Mwinyi akizungumza kwenye uzinduzi wa mpango wa utekelezaji wa afya za maradhi yasiyoambukiza (NCDs), hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Marlborough House nchini Uingereza. Mama Mariam alitoa wito huo wakati wa uzinduzi wa mpango wa utekelezaji wa afya za maradhi yasiyoambukiza (NCDs) unaolenga kutekelezwa katika nchi 56 wanachama wa Jumuiya ya Madola katika ukumbi wa Marlborough House, Uingereza. Alieleza kuwa ili kukabiliana na maradhi yasiyo ya kuambukiza kama ya saratani, ugonjwa ya moyo, shinikizo la damu na mengineyo hususani kwa vijana, kuna hitajika jamii kuhakikisha inapata lish...