Posts

Showing posts from July, 2023

Toeni taarifa za madhila mnayofanyiwa kazini – Simbaya

Image
NA MWANDISHI WETU MKURUGENZI Mtendaji wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Kenneth Simbaya (wa pili kushoto aliyeshikana mikono na Katibu wa KGPC - Mwajabu Hoza)  amewahimiza waandishi wa Habari kutoa taarifa za madhila wanayofanyiwa wanapokua kazini ili hatua zichukuliwe. Simbaya alitoa wito huo mkoani Kigoma alipokua akizingumza na waandishi wa habari wanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani humo (KGPC), alipofika kujitambulisha kwa wanachama na kueleza mipango ya utekelezaji wa mpango wa mkakati wa UTPC wenye kaulimbiu ya ‘Kutoka kwenye ubora kwenda kwenye ukubwa (Moving from good to great). Mkurugenzi huyo aliyembatana na Ofisa Programu, Mafunzo, Utafiti na Machapisho, Victor Maleko, alisema hatua hiyo itapunguza vitendo hivyo vinavyopunguza uhuru wa vyombo vya habari nchini. MKURUGENZI Mtendaji wa Muungano wa klabu za waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Kenneth Simbaya (wa pili kushoto) akieleza jambo kwa Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Hab

Dk. Mwinyi ahimiza malezi bora ya watoto, vijana

Image
NA MWANDISHI MAALUM, PEMBA RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi ameihimiza jamii kuweka mkazo kwenye malezi ya watoto na vijana ili kukuza taifa lenye maadili, nidhamu na kizazi chema chenye kumjua Mwenyezi Mungu. Dk. Mwinyi aliyasema hayo kwenye kilele cha maadhimisho ya mwaka mpya wa Kiislamu Zanzibar 1445 Hijria yaliyofanyika katika Masjid Munawwara, Mfikiwa  mkoa wa Kusini, Pemba. Alisema ni wajibu wa wazazi na walezi kuwasimamia vyema watoto wao na kuwapa elimu ya dini na dunia ili kuwaepusha na vitendo vya uvunjivu wa amani, tabia mbaya na vitendo vya udhalilishaji. Akizungumzia historia ya tarehe ya Kiislaam, Alhajj Dk. Mwinyi alieleza ilianza mara baada ya  Mtume SAW kuhama Makka na kuhamia Madina ambako utulivu na Amani ulipatikana na kuwa chanzo cha kuenea uislam dunia nzima. Alisema lengo la kuadhimishwa mwaka Mpya wa Kiislam 1445 H ni kuendelea kusisitiza na kuhimiza amani, ushirikiano na upendo kwenye jamii Katika k

Dk. Mwinyi abainisha kipaumbele cha SMZ

Image
NA MWANDISHI WETU RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussain Ali Mwinyi, amesema sekta ya elimu ni miongoni mwa vipaumbele vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mujibu wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2020 - 2025.  Dk. Mwinyi aliyasema hayo alipoweka jiwe la msingi wa ujenzi wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Kampasi ya Pemba eneo la Mtima shehia ya Pujini, Wilaya ya Chake Chake, mkoa wa Kusini Pemba. Aliupongeza uongozi wa chuo hicho kwa kuona umuhimu wa kufungua Kampasi hiyo kisiwani Pemba ikiwa ni sehemu sahihi ya kusogeza huduma za jamii ikiwemo kutanua fursa zaidi za elimu kwa watu wa Pemba na Watanzania kwa ujumla. Aidha Dk. Mwinyi alisema serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa unaotolewa na Chuo hicho kwa kutoa mafunzo mbali mbali zikiwemo ngazi za Astashahada, Stashahada, Shahada na Shahada ya Uzamili. Alisema, pamoja na mafunzo ya ngazi hizo za kielimu, Chuo pia kimekuwa na mchango mkubwa kwa kutoa mafunzo ya Uongozi, Maadili na

Maonesho ya nane nane kuinua kilimo Zanzibar - Shamata

Image
NA MWANDISHI WETU WIZARA ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Misitu imeeleza kuwa itaendelea kutumia mbinu mbali mbali kushajihisha jamii hasa vijana na wanawake kushiriki kwenye kilimo ili kupunguza changamoto ya ukosefu wa ajira nchini. Waziri wa wizara hiyo, Shamata Shaame Khamis, alieleza hayo jana huko Dole, wilaya ya Magharibi ‘A’ Unguja, alipokua akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maonesho ya Siku ya Wakulima (nane nane) yatakayofanyika katika viwanja vya Dole Kizimbani mwezi ujao. Shamata alieleza kuwa maoenesho hayo limekua jukwaa muhimu kwa wakulima na wadau wa sekta ya kilimo kupata taarifa, maarifa na ujuzi unaochochea ushiriki wao kwenye kilimo lakini pia kuongeza uzalishaji wa mazao hivyo kuifanya nchi kuwa na uhakika wa chakula. “Kupitia maonesho wadau watajifunza mbinu na teknolojia mpya za kuongeza uzalishaji lakini pia kujiunga na shughuli za kilimo na kuongeza mnyororo wa thamani ya mazao yanayozalishwa hivyo kukifanya kilimo kuendelea kuwa na tija kwa maisha

SMZ kujenga mahakama, miundombinu huduma za jamii

Image
NA MWANDISHI MAALUM, IKULU SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesema itazijenga upya mahakama zote za Zanzibar a kupitia bajeti ya mwaka wa Fedha, 2023/2024. Aidha, imeeleza dhamira yake ya kukamilisha miradi yote ya maendeleo ndani ya kipindi cha mwaka mmoja kwa sekta zote zikiwemo, afya, elimu, maji safi, miundombinu ya barabara, ujenzi wa ofisi  za serikali pamoja na sekta ya michezo. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi aliyasema hayo aliposhuhudia utiaji wa saini  mkopo wa shilingi bilioni 470 zilizotolewa na benki ya NBC na benki ya NMB kwa upannde mmoja na Wizara ya Nchini Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango hafla iliyofanyika Ikulu, Zanzibar. Dk. Mwinyi amesema hii ni mara ya kwanza kwa SMZ kukopa Fedha kutoka benki za ndani na kuahidi kuzirejesha fedha hizo kwa kipindi kifupi kwani Serikali inauwezo wa kufanya hivyo na sasa inaakiba ya kurejesha gharama nusu za mkopo huo. Dk. Mwinyi alisema Fedha hizo zimekusudiwa kukamilisha miradi y

ZALIRI, FLI zaingia makubaliano kuimariusha sekta mifugo

Image
NA MWANDISHI MAALUM, WKUMM WIZARA ya Kilimo Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo imeeleza kuwa itaendelea kushirikiana na wadau mbali mbali kupitia taasisi zake kustawisha sekta ya kilimo na ufugaji. Waziri wa wizara hiyo, Shamata Shaame Khamis alieleza hayo baada ya kushuhudia utiaji saini ya makubaliano ya ushirikiano na kiutendaji kati ya Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Zanzibar (ZALIRI) na taasisi ya Friedrich Loeffler Institut (FLI) ya nchini Ujerumani.  Katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa ZARILI, Talib Saleh Suleiman alitia saini kwa niaba ya taasisi hiyo na kwa upande wa  FLI, Mkurugenzi wa Institute of International Animal/One Health, Prof. Sascha Knauf aliiwakilisha taasisi yake. Waziri Shamata  alieleza kuwa  serikali ya Ujerumani imekuwa na ushirikiano wa karibu na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi  Zanzibar katika mipango yake ya maendeleo.  Alifahamisha kuwa utiaji saini huo utaongeza ufanisi na wataalamu wa utafiti wa masuala ya mifugo lakini

Dkt. Mwinyi ahimiza ubunifu huduma za bima ZIC

Image
NA MWANDISHI WETU RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi (wa pili toka kulia) amezindua huduma ya bima inayofuata misingi ya dini ya Kiislamu (Takaful) inayotolewa na Shirika la Bima Zanzibar (ZIC) na kulipongeza shirika hilo kwa ubunifu wa huduma hiyo hiyo itakayowavutia wananchi waliokua wakiepuka huduma za bima kwa mitazamo ya imani ya kidini . Uzinduzi huo ulifanyika jijini Zanzibar Julai 5, mwaka huu ambapo huduma hiyo itakuwa inatolewa na ZIC kupitia kampuni yake tanzu inayofahamika kama ZIC Takaful ambapo dkt. Mwinyi alisisitiza azma ya serikali ya mapinduzi Zanzibar kuhakikisha huduma za bima zinawafikia wananchi wote bila ya vikwazo vya kiimani bali matakwa yao. Dkt. Mwinyi akizungumza na watendaji wa ZIC na wadau mbali mbali wa huduma hiyo wakiwemo viongozi wa serikali, dini, wadau wa bima, taasisi za fedha na wananchi, amesema huduma hiyo imekua ikitolewa maeneo mbali mbali ulimwenguni hivyo itaongeza sifa za uwekezaji nchini. “Kwa muda mr

Kheri ya Siku ya uhuru wa USA

Image
 

Wahariri chachu ya maendeleo, ukuaji wa Kiswahili - Hemed

Image
NA MWANDISHI WETU MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, ameeleza kuwa juhudi za wahariri wa vyombo mbali mbali vya habari zimechangia ukuaji na maendeleo ya lugha ya Kiswahili ulimwenguni. Hemed ameyasema hayo katika mkutano wa wahariri wa vyombo vya habari wa Tanzania kuadhimisha Siku ya Kiswahili Duniani uliofanyika ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil Kikwajuni jijini Zanzibar. Amesema Wahariri Wakuu wana jukumu la kupitisha na kuweka sawa maandishi yote ndani ya vitabu, magazeti, majarida na vipindi vya redio au televisheni hatua iliyosaidia kwa kiasi kikubwa kukuza lugha hiyo ndani na nje ya Tanzania. Aidha   amewataka kuendelea kuzingatia maadili ya kazi zao na kuibua mambo yasiyoendana na mila, tamaduni na silka za nchi bila ya kumuonea mtu au taasisi muhali. Hemed pia alitumia jukwaa hilo kueleza fursa zinazopatikana katika lugha ya Kiswahili na kuwataka wenye ujuzi wa lugha hiyo kuzichangamkia ikiwemo ukalimani, utafsiri, uhariri, uandishi na utan