Dk. Mwinyi aeleza dhamira CCM kufanya vikao vikuu Z'bar

NA MWANDISHI WETU MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi ameahidi kuwa chama hicho kitafanya mkutano mkuu wake taifa ndani ya visiwa vya Zanzibar ilimkutoa fursa kwa wajumbe kushuhudia maendeleo yaliyopatikana. MAKAMU Mwenyekit wa CCM Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi, akisalimiana na mmoja ya wenyeviti wa CCM wa mikoa waliofika ikulu kumsalimia. Dk. Mwinyi ambaye pia ni na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi aliyasema hayo Ikulu Zanzibar alipokua akizungumza na Wenyeviti wa mikoa wa chama hicho kutoka mikoa yote ya Tanzania waliofika kumsalimia. Alisema CCM Zanzibar, itahakikisha inalifanikisha azma hiyo na kuwezesha uptikanaji wa rasilimali zote ikiwemo eneo muafaka la kuhudumia wajumbe wote wa mkutano huo na mikutano mengine ya Halmashauri Kuu taifa ikiwa ni pamoja na kujenga ukumbi mkubwa wa mikutano. Alieleza kuwa uwepo wa ukumbi huo utaiwezesha nchi nzima kuwa Zanzibar ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya ...